Friday, May 5, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA SABA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 4, 2017.




unnamed
Mwenyekiti
wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge 
akiongoza kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

MHE.MHAGAMA




A 1
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali
imesema kuwa haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru
na kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi
kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.

TADB, SUA WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO




S
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Francis Assenga (katikati) akiongoza kikao cha majadiliano juu ya
ushirikiano na Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) wakati
uongozi wa Chuo hicho walipotembelea Ofisi za TADB. Msafara wa huo wa
Chuo cha Kilimo uliongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Susan
Nchimbi-Msolla (wapili kulia) na msaidizi wake Prof. Benard Chove
(kulia). Wengine pichani ni wajumbe wa menejimenti ya TADB.

WANAFUNZI ARUSHA WAPEWA ELIMU YA MADINI




Wanafunzi
wa Shule wa Sekondari ya Arusha wakimsikiliza Mkufunzi kutoka  Taasisi
ya  Gemological Insitute of America (GIA) , Elizabeth  Bokaba (hayupo
pichani). Wanafunzi hao wamepata mafunzo kuhusu mafunzo ya Jimolojia.
 


WANAFUNZI ARUSHA WAPEWA ELIMU YA MADINI




Wanafunzi
wa Shule wa Sekondari ya Arusha wakimsikiliza Mkufunzi kutoka  Taasisi
ya  Gemological Insitute of America (GIA) , Elizabeth  Bokaba (hayupo
pichani). Wanafunzi hao wamepata mafunzo kuhusu mafunzo ya Jimolojia.
 


WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA WALIVYOSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI DEI), UWANJA WA UHURU DAR ES SALAAM PAMOJA NA HAFLA YA KUTUNUKU WAFANYAKAZI HODARI






Aliyekuwa
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta  ambaye anajiandaa kustaafu,
Bw. Fortunatus Kapinga akizungumza wakati wa kuwatuza wafanyakazi hodari
wa shirika. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu mpya, Deo Kwiyukwa na
kulia ni Meneja wa Fedha, Cyprian Mugemuzi. Picha na Ismail Mang'ola.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA MAJI WA BILIONI 29 MKOANI TABORA



maj1
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata ya maelezo juu ya mradi wa maji vijijini  katika kijiji cha
Mabama,Wilaya ya Uyui mkoani Tabora kutoka kwa Katibu Tawala Msaidizi
Huduma ya Maji Mhandisi Muhibu Lubasa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)


maj2maj3
:Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wananchi wa kijiji cha Mabama waliojitokeza wakati wa
uzinduzi wa mradi wa maji vijijini mkoani Tabora uliofadhiliwa  na
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Japan (JICA).
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
maj4
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akifungua maji katika shule ya msingi ya Mabama wilaya ya Uyui kama
ishara ya usinduzi wa mradi wa maji vijijini.  (Picha kwa na Ofisi ya
Makamu waa Rais)
maj5maj7
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimtwisha maji mkazi wa kijiji cha Mabama kama ishara ya kuzindua maji
.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
maj8
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji vijijini mkoani Tabora
maj9
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na
viongozi wengine  wakipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi
kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji vijijini mkoani Tabora
maj10
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji vijijini
mkoani Tabora
maj11
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuweka 
jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji vijijini mkoani
Tabora.
Q 1

 
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Serikali
imezindua mradi wa ujenzi na usambazaji maji vijijini wenye thamani ya
shilingi bilioni 29 katika Halmashauri saba za mkoani Tabora.

Mradi
huo umezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Kijiji cha Mabama Wilayani Uyui
mkoani Tabora.

Ujenzi
wa Mradi huo umefadhiliwa na Japan kupitia  Shirika la Maendeleo la
Japan (JICA) ambao umewezesha uchimbaji wa visima 111 na ujenzi wa
mitandao minne ya bomba.

Akizungumza
na wananchi wa Mabama mkoani Tabora wakati wa sherehe za uzinduzi wa
mradi huo Makamu wa Rais huyo alisema kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu
ya mpango wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wengi hapa nchini na wale
wa mkoa huo wanakuwa na uhakika wa huduma ya maji safi na salama.

Alisema
kuwa lengo la Serikali ni kuendelea na jitihada kuwajenga miradi
mbalimbali wananchi kwa nguvu zake na wakati mwingine kwa kushirikiana
na wahisani.

Mhe.
Samia alisema kwa kuwa mradi huo utawanufaisha wanachi wapatao 40,352
katika vijijini 31 vya Mkoa wa Tabora ni vema wananchi wakautunza ili
uweze kutumika kwa muda mrefu.

Aliwaasa
wanufaika wa mradi huo maji vijijini kutoharibu miundo mbinu za visima
na bomba ili uweze kusaidia kuwaondolea adha wananchi na hasa wakinamama
na watoto wa kike ambao walikuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji
badala ya kushiriki katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Aidha
, Makamu huyo wa Rais ametoa kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya
maji ili jamii iendele kunufaika na rasimali hiyo muhimu kwa uhai wa
wanandamu na maendeleo mengine.

Aidha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano huyo ameishukuru serikali ya
Japani kwa msaada huo ambao ni ukumbozi kwa wakazi wa Tabora.

Hivyo
kufuatia hali hiyo aliwaagiza viongozi kuanzia ngazi ya chini hadi Mkoa
kutomfumbia macho mtu anayeharibu mazingira kwa makusudi na ikiwezekana
hatua kali zoichukuliwe dhidi yake.

Naye
Balozi wa Japani hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema kuwa Japan
itandelea kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa miradi mbambali hapa
nchini kwa lengo la kuwaletea huduma wananchi kwa karibuni.

Alisema
kuwa ujenzi wa mradi huo ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo mbaina
ya Tanzania na Japan na kuahidi kuendelea na ushirikiano huo.

Awamu
Mkuu Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alitoa salamu za Mkoa alisema
kuwa uharibifu wa mazingira mkoani huo kwa sababu za kilimo cha tumbaku
kisichozingatia matumizi madogo ya kuni na ufugaji wa usiozingatia
utunzaji wa mazingira umesababisha upungufu wa mvua mkoani huo.

Alisema
kuwa wakati mazingira mkoani bado hayajaharibiwa mkoa huo ulikuwa na
uwezo wa kupata mvua kufikia milimita 1800 lakini hivi sasa Tabora
inapata mvua ambazo ni milimita 650.

Mkuu
huyo wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo la
uharibifu wa Mazingira, viongozi mbalimbali wa mkoani huo wameendesha
kampeni ya kupata miti katika maeneo yote kwa kutumia teknolojia ya
matone.

Naye
Waziri wa  Maji na Uwagiliaji Greyson Lwenge alitoa wito kwa
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote hapa nchini kuanzisha miradi
ya uchumbiaji wa mabawa madogo madogo kwa ajili ya kukabiliana na tatizo
la maji katika maeneo yao.

Alisema
kuwa Wizara hiyo itaendelea na jitihada zake za utatizi wa kero ya maji
, lakini vema na Halmashauri zitafuta njia za kuwaondolea wananchim
kero hiyo.

Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban alisema kuwa
mradi huo umekuwa mkombozi kwa baadhi ya wakazi wa mkoa wa Tabora na
hasa Halmashauri yake kwa kuwa walitumia muda mwingi na fedha nyingi
kununulia maji.

Alisema
kuwa baada kujengwa mradi huo hivi sasa wananchi wananunua dumu moja la
lita ishirini kwa shilingi 50 wakati hapo awali walikuwa wakinunua kwa
kiwango cha kuanzia shilingi 500 hadi 1,000 wakati wa kiangazi.

Mwenyekiti
huyo alisema kuwa mradi huo pia umesaidia kupunguza muda mwingi ambao
wakinamama waliupoteza kutafuta maisha badala ya kwenda kuzalisha mali.

Aliongeza kuwa faida nyingine ni kuwa mradi huo umesaidia kurudisha mahusiano katika familia.
Q 1