Friday, May 5, 2017

 
DAWASCO inatambua na kuthamini sana
juhudi zinazofanywa na wadau wote wa
huduma zinazotolewa na Shirika tukiamiani
kuwa tunaweka nguvu za pamoja zinazolenga
kukabiliana na changamoto kubwa za
kiuendeshaji na kiuwekezaji kwa lengo la
kuboresha huduma ya maji safi na uondoshaji
wa majitaka jijini Dar es Salaam na miji ya Kibaha
na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Miongoni mwa changamoto za kiuwekezaji
ambazo zimekuwa zikikwamisha huduma ya
maji katika maeneo yanayopata huduma kutoka
DAWASCO ni pamoja na kiwango cha maji
yanayozalishwa kwa siku kutotosheleza mahitaji,
Upotevu wa maji na Uchakavu wa Miundombinu.
Katika kupambana na changamoto hizo
DAWASCO ikishirikiana na DAWASA na Wizara
ya Maji, imeanza hatua za utekelezaji wa mikakati
ya kuondoa kero inayowakabili watumiaji wa
huduma kwa kuanza kwa ujenzi wa miradi
ya kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita
za ujazo 300,000 mpaka kufi kia mita za ujazo
710,000 kwa siku, ikizingatiwa kuwa makadirio
ya matumizi ya maji kwa siku ni mita za ujazo
450,000 kwa siku.
Mkakati huu unahusisha upanuzi wa mitambo
ya kuzalisha Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini,
Uchimbaji wa visima 20 katika maeneo ya Kimbiji
na Mpera, ujenzi wa Bwawa la Kidunda Mkoani
Morogoro na mradi wa kupunguza upotevu wa
maji toka asilimia 48 hadi asilimia 20.
Kazi ya upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini
inaendelea na baada ya kukamilika utaongeza
uzalishaji toka mita za ujazo 182,000 hadi mita
za ujazo 270,000 kwa siku.Upanuzi wa Mtambo
wa Ruvu Juu utaongeza uzalishaji toka mita
za ujazo 81,000 mpaka za ujazo mita za ujazo
196,000 kwa siku, wakati visima virefu peke yake
vitaweza kuzalisha mita za ujazo 260,000 kwa
siku. Mipango yote hii ipo katika utekelezaji na
hivyo kuweka tumaini la kutoa huduma bora na
ya uhakika ifi kapo Disemba 2014.
Ujenzi wa bwawa la kuhifadhia Maji Kidunda
Mkoani Morogoro wenye uwezo wa kuhifadhi
hektomita za ujazounalenga kuhakikisha
upatikanaji wa Maji katika vipindi vyote vya majira
ya mwaka. Hii itasaidia kukabiliana na tatizo la
kupungua kwa kina cha Maji katika mto Ruvu
hasa kipindi cha Kiangazi.
Tunawasihi wananchi waendelee kuitunza,
kuilinda na kuhifadhi Miundombinu yote ya maji
iliyopo katika maeneo yao
Katika utoaji wa huduma za kila siku, Shirika
linakabiliana na changamoto kubwa zifuatazo;
Gharama za kubwa nishati ya umeme na
madawa ya kutibu maji, maji kutotosheleza
mahitaji, upotevu wa maji, hujuma kwenye
miundombinu ya maji safi na majitaka kama vile
wizi wa maji na wizi wa mifuniko ya chemba za
majitaka. Pia wateja kutolipia ankara kwa wakati,
maji kupatikana kwa mgawo na maeneo mapya
kutokuwa mabomba ya usambazaji.
Katika kukabiliana na changamoto hizi za
uendeshaji, DAWASCO inasimamia na
kutekeleza majukumu yake kwa kuzishirikisha
Serikali za mitaa, wateja na wadau wengine
wa Maji katika kulinda, kutunza na kuhifadhi
Miundombinu ya Maji ili isiharibiwe au kuibiwa.
Kwakuwa asilimia 13 tu ya jiji la Dar es Salaam
ndio inayopata huduma ya majitaka na hivyo
ipo mikakati ya kupanua huduma hii muhimu na
ustawi wa jiji la Dar es Salaam. Katika hili Shirika
lina mkakati wa kujenga mitambo maalumu ya
kusafi sha Majitaka katika maeneo ya Jangwani,
Kurasini na Mbezi Beach.
Mpango huu pia utahusisha ukarabati wa
miundombinu ya majitaka na kuendeleza juhudi
za kukemea na kuchukua hatua za kisheria
kwa wezi wa mifuniko ya chemba za majitaka
zinazosababisha kuziba na Majitaka kufurika
barabarani, kusababisha hatari kwa watumiaji wa
barabara na pia ni hatari kwa afya za wakazi.
DAWASCO inadhamiria kuleta mabadiliko ya
kiutendaji na kuboresha huduma kwa Umma
wa Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kibaha na
Bagamoyo Mkoani Pwani. DAWASCO ya sasa
imejipanga kutimiza wajibu wake kwa kusimamia
mikakati iliyojiwekea na hivyo wito unatolewa kwa
jamii kutimiza wajibu wake kwa kulipa ankara za
Maji kila mwezi ili kuliwezesha Shirika kuendesha
shughuli zake kwa ufanisi zaidi. DAWASCO
TUTAKUFIKIA
 
 

True value Media: TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI

                               TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI






TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI














 Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Meneja
Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali. Picha na Ismail Mang'ola.

SSRA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ILIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI KILIMANJARO




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Sara Kibonde Msika (wa kwanza kushoto), wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa SSRA katika banda la
Mamlaka hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
ambayo Kitaifa yalifanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi 
 mkoani Kilimanjaro.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakiwa kwenye banda la SSRA wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mkoani Kilimanjaro.

Wafanyakazi
wa 
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakipita mbele ya Mgeni Rasmi katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi
wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi),
zilizofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.


Wafanyakazi
wa 
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakipita mbele ya jukwaa kuu katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi
wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi),
zilizofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
 


Wafanyakazi
wa SSRA wakiwa katika maandamano wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Mkoani Kilimanjaro.
 


Wafanyakazi
wa SSRA wakimsikiliza kwa makini mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yalizofanyika
Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
 


Wananchi
wakiwa katika banda la SSRA wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi
Duniani (Mei Mosi) yalizofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika
Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea banda la SSRA wakipata vipeperushi vya Mamlaka hiyo
wakati wa Maadhimisho ya
  Siku
ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yalizofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Chuo
cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro


Wadau
wakipata maelezo kuhusu Hifadhi ya Jamii kutoka Maofisa wa SSRA wakati wa sherehe ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Picha na Ismail Mang'ola.

TGNP YAENDESHA SEMINA KUJADILI VIPAUMBELE KATIKA BAJETI YA WIZARA YA AFYA YA MWAKA 2017/2018





 Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha
wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es
Salaam jana.
 Mdau  Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.
 Anna Sangai akichangia jambo kwenye semina hiyo.
 Sadick Juma mkazi wa Mbezi Beach,
akielezea changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika
Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.
 Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matibabu ya homa ya ini ambayo dawa zake hazipatikani nchini hadi zitoke India.
 Moses Benard akizungumzia wajawazito
kujinunulia vifaa vya kujifungulia na suala la dawati la ukatili wa
kijinsia kuwepo vituo vya polisi.
 Mdau Dalia Kalungwana akichangia jambo.
 Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
 Semina ikiendelea.
 wananchi wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
Vijana wakifuatilia mada katika semina hiyo.

Na Ismail Mang'ola

WANANCHI wameiptia bajeti ya mwaka
2017/ 2018 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
iliyotengwa na kuomba iongezwe kwa kuzingatia ukubwa wa wizara hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti
katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania
(TGNP) ya majadiliano ya kupitia bajeti hiyo ili kuona vipau mbele
vyake waliombwa iongezwe ili iweze kukabiliana na changamoto zilizopo
kwenye wizara hiyo ambayo imelemewa kutokana na ukubwa wake.

Kwa
mwaka wa fedha wa 2016/ 2017 wizara hiyo ilitengewa bajeti ya sh.bilioni
845 ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambapo 
Jumla kuu ya fedha zote zinazoombwa kwa Wizara hiyo ni Sh. 1,115,608,772,090.00.

Akizungumza katika semina hiyo,
Neofita Kunambi alisema katika wizara hiyo kunachangamoto kubwa bila ya
kuongezewa fedha katika bajeti yake hazitaweza kuisha.

"Bila ya kuongeza bajeti katika
wizara hii wajawazito wataendelea kujinunulia vifaa vya kujifungulia
tunaomba jambo liangaliwe kwa karibu" alisema Kunambi.

Anna Sangai alisema huduma za afya
zinapaswa kuboreshwa kuanzia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na bila
kuongezwa kwa bajeti katika wizara hiyo itakuwa ni ndoto.

Mkazi wa Mbezi Beach, Sadick Juma
alisema upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, miundombinu na ukatili wa
kijinsia ni changamoto kubwa katika wizara hiyo.

Alisema licha ya kuwepo duka la
Bohari ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili
(MNH), upatikanaji wa dawa umekuwa mgumu hivyo kuifanya Muhimbili kuwa
na majengo mazuri bila ya kuwa na dawa.

"Ukitaka kuona changamoto hata ukiwa
ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ugua au uwe na
mgonjwa ambaye ni mwanachama uende katika hospitali hiyo kwanza
kupokelewa tu pale mapokezi ni balaa na ukifika muda wa kutakiwa kupata
dawa utaambulia panado na kuambiwa dawa hazipo" alisema Juma.

Juma aliongeza kuwa huduma ya bure
kwa watu wenye msamaha hiyo ni ndoto kwani wagonjwa hao hawasikilizwi
kabisa jambo ambalo ni hatari.

Alisema serikali imekuwa ikijipodoa
kuwa inaboresha huduma za afya lakini hali halisi haipo hivyo akitolea
mfano kwa nchi nzima maduka ya dawa ya MSD yapo nane tu je upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba utafikia katika kiwango cha kukidhi mahitaji
alihoji Juma.

Janeth Mawinza alisema bajeti hiyo
iangalie zaidi jinsi ya kutibu magonjwa kama ya homa ya ini ambayo
matibabu yake kwa hapa nchini hayapatikani mpaka dawa itoke nchini
India.

Moses Benard alisema ikiwa mjamzito
aliopo mjini anatakiwa kujinunulia vifaa vya kujifungulia hali ikoje kwa
yule ambaye yupo kijijjini ambaye anachangamoto ya kutokuwa na fedha na
kukimbiwa na mwenza wake hivyo akaomba Waziri wa wizara hiyo kutoa
tamko rasmi la kuwataka wajawazito kutonunua vifaa hivyo wanapokwenda
hospitali kujifungua.

Wadau wengine waliongelea jijini Dar
es Salaam maeneo mengine kama Kipunguni wilayani Ilala kukosa kuwa na
zahanati au hospitali hivyo kulazimika kwenda wilaya ya Kisarawe kupata
matibabu jambo ambali linashangaza hivyo wakaomba bajeti ya wizara hiyo
iongezwe ili kufanikisha upatikanaji wa zahanati au hospitali katika
maeneo yao.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA SABA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 4, 2017.




unnamed
Mwenyekiti
wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge 
akiongoza kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

MHE.MHAGAMA




A 1
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali
imesema kuwa haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru
na kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi
kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.