Wednesday, June 14, 2017

True value Media: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BU...

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA

 Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa
Saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angeline Kairuki akijibu maswali mbalimbali
ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini
Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na
Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika
kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akifuatilia jambo na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Suzan Kolimba  hoja
mbalimbali za wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana  Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera ,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama akizungumza jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao
cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mhe.Fatma Toufiq akiuliza swali
katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni
13, 2017.
 Mbunge wa Viti maalum (CCM)
Mhe.Ritta Kabati akiuliza swali katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa
Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akiwa katika picha ya
pamoja na wanakwaya wa Furahini K.K.K.T Ilongero-Mijuhu Singida  Bungeni
Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia
Wambura akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kwaya ya Furahini K.K.K.T
Ilongero-Mujuhu Singida walipokuja kumtembelea Bungeni mjini Dodoma.

Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

MAJALIWA AWAVALISHA VYEO MAAFISA WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS

MAJALIWA AWAVALISHA VYEO MAAFISA WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa
Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja
wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni
12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli
katika hafla hiyo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile
Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga
jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha
Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . 
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye
uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam
Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe
Magufuli katika hafla hiyo .

 Manaibu Kamishina  wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya
Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu,
Kasim Majaliwa aktika hafla fupi  iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha
Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla
hiyo. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya
kuvalisha vyeo Maafisa magereza  iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha
Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.
Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla
hiyo. 

 Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya
 kuwavalisha Vyeo Maafisa Magereza kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa
mahaliwa alimwakisha Rais John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na
Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe
Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga
jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017.

 (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA

 Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa
Saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angeline Kairuki akijibu maswali mbalimbali
ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini
Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na
Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika
kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akifuatilia jambo na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Suzan Kolimba  hoja
mbalimbali za wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana  Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali
mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera ,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama akizungumza jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao
cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mhe.Fatma Toufiq akiuliza swali
katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni
13, 2017.
 Mbunge wa Viti maalum (CCM)
Mhe.Ritta Kabati akiuliza swali katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa
Bunge la 11  Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akiwa katika picha ya
pamoja na wanakwaya wa Furahini K.K.K.T Ilongero-Mijuhu Singida  Bungeni
Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia
Wambura akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kwaya ya Furahini K.K.K.T
Ilongero-Mujuhu Singida walipokuja kumtembelea Bungeni mjini Dodoma.

Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

MD KAYOMBO: MIL 85,000,000 ZAPATIKANA ZITAJENGA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI HONDOGO

MD KAYOMBO: MIL 85,000,000 ZAPATIKANA ZITAJENGA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI HONDOGO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 14,
2017 Ameeleza dhamira yake kuhusu ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa
katika shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba.

True value Media:    MTOTO WA MIAKA 12 KUTOKA SOMALIA ANYAKUA MI...

YANGA YASAJILI BEKI KISIKI KUTOKA  ZANZIBAR

3

Mabingwa mara tatu mfululizo wa
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ‘VPL’, Yanga SC, wameanza kufuru ya
usajili baada ya kunasa beki kisiki toka visiwani Zanzibar
Mlinzi mahiri wa Timu ya Taifa ya
Jang’ombe ya Zanzibar, Abdallah Haji Shaibu maarufu kwa jina la “Ninja”
amesaini mkataba wa miaka miwili (2) kuichezea Yanga.
Pichani, katibu mkuu wa Yanga,
Charles Mkwasa (kushoto) akimsainisha leo Abdallah Haji (kulia) ofisini
kwake Makao makuu ya Yanga, Mtaa wa Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam.

Monday, June 12, 2017

QU1

 Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa
akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi
Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Juni 11, 2017

QU2

 Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa
akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi
Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Juni 11, 2017. 

QU3

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi
milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya
Kuhifadhi  Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam Juni 11, 2017. 

QU5

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Paul Makonda  akizungumza katika mashindano hayo 
yaliyofanyika kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.

QU6

Rais Mstaafu wa Awamu ya  Pili na
Mlezi wa Taasisi ya Al- Hikima Foundation, Alhaj Ali Hassan Mwinyi
akizungumza katika  kilele cha Mashindano ya 18 ya Kuhifadhi Qur-an
Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni
11, 2017. 

QU7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiteta na Mufti na  Sheikh Mkuu wa Tanzania  Sheikh Abubakr Zubeir bin
 Ally (kulia) na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye
ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi
hiyo , katika  Mashindano ya 18 ya Afrika ya  Kuhifadhi Qur-an Tukufu
 yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11,
2017.
Picha zote na Ismail Mang'ola

QU8
Na Ismail Mang'ola

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiteta na Mufti na  Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar
ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na Mlezi Mwenza wa
Taasisi hiyo, katika  Mashindano ya 18 ya Afrika ya  Kuhifadhi Qur-an
Tukufu  yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni
11, 2017. 

Mtoto wa miaka 12 kutoka Somalia,
Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani
7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika Mashariki ya
kuhifadhi na kusoma Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.

Mohammed ambaye ni miongoni mwa
washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi),
amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait,
ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na
ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus
Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na maelfu ya waumini
na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
leo mchana (Jumapili, Juni 11, 2017), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
waandaaji wa mashindano hayo ambayo ni Taasisi ya Al-Hikma waangalie
uwezekano wa   kuboresha zawadi kwa kutoa scholarships udhamini kwa washindi au washiriki, ambao ni kwa washiriki wa Tanzania.

“Ongeeni na nchi marafiki kama
Saudi Arabia, waone uwezekano wa kutoa zawadi za ufadhili kwenye masomo
ya sekta za kimkakati kama vile mafuta na gesi, ili kuongeza hamasa na
chachu ya vijana walioko kwenye sekondari zetu nao waone fursa hii na
kuichangamkia, badala ya mashindano kujikita kwenye madrasa peke yake,”
amesema.

Waziri Mkuu amewataka wazazi
wafuatilie nyendo za vijana wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa
za kulevya na vitendo vingine viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao
na ustawi wa nchi yetu lakini akasisitiza pia waisaidie Serikali katika
mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi.

“Endeleeni kushirikiana na
Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi na kuwafichua
wakwepa kodi, kila mmoja wetu ahakikishe analipa kodi stahiki kwa mujibu
wa sheria, hii itasaidia Serikali kuboresha huduma kwa wananchi ili
waweze kufanya ibada zao vizuri zaidi,” amesema.

Washindi wengine kwenye kundi
hilo na umri wao kwenye mabano ni Abdulkarim Ahmed Farhina (22) wa Sudan
ambaye ameshinda dola za Marekani 5,000, cheti, IPAD, kompyuta
iliyotolewa na Balozi wa Kuwait ametoa ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wa tatu ni Mahamoud Ali Chamfi wa
Comoro (18) na Seif Ramadhani Zombe (18) kutoka Taasisi za Tanzania
ambao wote wamepata dola za marekani 3,000, cheti, IPAD, kompyuta
iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wa nne ni Khalil Mussa Hussein
(17) kutoka Tanzania Bara ambaye amepata dola za marekani 1,500, cheti,
IPAD, na ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam. 

Wa tano ni Ismail Issa Qasim (17) kutoka Tanzania Visiwani
ambaye dola za marekani 1,000, cheti, IPAD, na ahadi ya sh. milioni moja
kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,

Washiriki wengine kwenye kundi la
juzuu 30 walitoka nchi za Nigeria, Kenya, Uganda, Djibouti, Afrika
Kusini, Rwanda, Ghana, Ethiopia, Congo DRC, Burundi na Msumbiji. Umro
wao ulikuwa ni kati ya miaka 12 na 26.

Washiriki wengine waliopewa
zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watano), Juzuu
tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi
watatu).

Viongozi wengine waliohudhuria
kilele hicho ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Balozi wa Saudi Arabia nchini
Tanzania, Mhe. Mohamed Bin Mansour Al Malek.

 Wengine ni wawakilishi
wanne wa Imam Mkuu wa Mskiti Mtakatifu wa Makkah, Sheikh Abdul Rahman
Ibn Abdul Aziz as-Sudais; Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh
Abubakar Zubeir bin Ally na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh
Alhad Mussa.

Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amemuagiza Meya wa Temeke, Bw. Abdallah Chaurembo kesho (Jumatatu,
Juni 12, 2017) afuatane na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bw. Nassib
Mmbaga hadi kwenye kiwanja kilichopo eneo la Matumbi na kukagua kama
kuna uwezekano wa kuliongeza kwa taasisi ya Al-Hikma na wampe majibu
Jumanne kwani limekaa wazi kwa muda mrefu licha ya kuwa walishaliomba na
hawakupata majibu.

“Mstahiki Meya wa Temeke na
Mkurugenzi wako, kesho Jumatatu nendeni mkaangalie eneo husika kama
linafaa kuongezwa na mfanye maamuzi. Eneo hilo limekaa wazi kwa muda
mrefu, na hawa wanataka wanataka kujenga zahanati. Jumanne asubuhi
nipate taarifa ya maamuzi yenu,” alisema Waziri Mkuu na kushangiliwa na
maelfu ya waumini waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

Tuesday, June 6, 2017

True value Media: True value Media: CCM WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HA...

OFISI
YA TAIFA YA TAKWIMU YAENDESHA MAFUNZO KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA
MATUMIZI YA KAYA BINAFSI TANZANIA BARA WA MWAKA 2017/18

unnamed

Mkufunzi anayesimamia mafunzo ya
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18 (2017/18 HBS) Sergiy Redyakin akimwelekeza mmoja wa washiriki wa
mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) namna ya kujaza
dodoso litakalotumika katika utafiti huo unaotarajia kufanyika nchini
kuanzia mwezi Agosti, 2017.
1
Baadhi ya Watakwimu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na
mkufunzi anayesimamia mafunzo hayo Sergiy Redyakin (hayupo pichani)
wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 yaliyofanyika hivi karibuni katika makao
makuu ya NBS Dar es Salaam.
2
 Baadhi ya watakwimu kutoka NBS
wakijifunza namna ya kujaza madodoso kwa njia ya kieletroniki wakati wa
mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara
wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti,
2017.
3
 Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Hellen Mtove (wa kwanza kulia) akimhoji mmoja wa wanakaya
wakati wa majaribio ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia
mwezi Agosti, 2017.