Wednesday, September 9, 2015

True value Media: True value Media: MSIMAMO MEDIA .COM: True value M...














NGOMA AFRICA BAND KUVAMIA MARBELLA – SPAIN JUMAMOSI 12 SEPT 2015

unnamedBendi
maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-
Ughaibuni inatategemewa kufanya onyesho maalumu katika Grande VIPsiku ya
jumamosi 12 Septemba 2015,kule katika kisiwa cha mabwanyenye
Marbella,kilichopo Spain. bendi hiyo imealikwa na VIP Yatch Club ya
Marbella.
Usikose kuungana nao 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA, MJINI KIGOMA LEO.

07
Waziri wa Nchi- Uwekezaji na
Uwezeshaji, Eng. Christopher Chiza, akizungumza kabla ya kumkaribisha
Mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dkt. Bilal ili kufungua Kongamano hilo.
Picha zote na OMR
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati
akifungua rasmi Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika
leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
06
Mwakilishi wa Umoja wa wafanyabishara wa Burundi, akizungumza.
04
05
Sehemu ya washiriki wa Kongamano
hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia
kwenye ufunguzi wa Kongamano hilo.
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya
jiwe lenye Madini huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni
ya Aifola Investiment Co. Ltd, Zubery Mabie, kuhusu upatikanaji wa
madini na utengenezaji wa Unga wa ‘Lime Powder’, wakati Makamu alipokuwa
akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la
Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye
Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka
kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Samaki wa Mapambo, Nunu Mrisho, kuhusu
upatikanaji wa Samaki hao na soko lake , wakati Makamu alipokuwa
akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la
Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye
Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
     08
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi na Balozi waliohudhuria Kongamano hilo
baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
09
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Kamati ya Ulinzi
na Usalama wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Kongamano hilo baada ya
ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015.
010
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo
waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9,
2015.

ZOEZI LA KUWASAJILI WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI LAENDELEA KATIKA KAMBI YA NYARUGUSU ,WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA

1
Mtoto Baraka Dombeni, akiwa na
mama yake Bizimana Violet, akivishwa alama ya utambuzi muda mfupi baada
ya kuwasili jana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, akitokea Wilaya
ya Makamba nchini Burundi. Alama hii ni utambulisho wa kuwawezesha
wakimbizi wanaofika katika kambi ya Nyarugusu kuandikishwa rasmi kabla
ya kupewa hifadhi kambini hapo.
2
Afisa Msajili Msaidizi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi (UNHCR), Awadhi Nyanda
akichukua taarifa toka kwa familia mojawapo ya wakimbizi kutoka Burundi
wanaoendelea kuingia nchini kuomba hifadhi. Wakimbizi hawa wanahifadhiwa
katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu Mkoani
Kogoma.
3
Mkimbizi kutoka Burundi, Sindaye
Salvatory akiwa na wenzake, akiwekewa alama yake ya utambulisho, wakati
walipowasili katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu jana, wakitokea
nchini Burundi kuja kuomba hifadhi nchini Tanzania kutokana na hali ya
kisiasa nchini mwao.
4 
Afisa wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, Vivian Vianney akimchukua alama za
vidole mkimbizi kutoka nchini Burundi Bw. Gwasa Jeremia ambaye ni
mmojawapo ya raia wa Burundi wanaoendelea kuingia nchini kuomba hifadhi
katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani
Kigoma.
6
Mwakilishi wa Shirika la OXFAM
toka nchini Ireland, Michaelo Riorpan akisaini kitabu cha wageni
alipowasili na wenzake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu jana.
Shirika la OXFAM linatoa misaada mbalimbali kusaidia utoaji wa huduma za
maji na utunzaji wa mazingira katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.
Aliyesimama ni Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B) Bw. Fredrick Nisajile
ambaye aliupokea ugeni huo.
7
Mkimbizi kutoka Burundi akipata
huduma ya maji katika moja ya vituo vya maji vilivyojengwa katika Kambi
ya wakimbizi ya Nyarugusu. Huduma za maji safi na salama ni mojawapo ya
mambo yanayotiliwa mkazo ili kulinda afya za wakimbizi.
5
Maofisa wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wanaohusika na usajili wa
wakimbizi wanaopokelewa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarutgusu, wakiwa
katika picha ya pamoja katika Kambi hiyo iliyoko wilayani Kasulu mkoani
Kigoma.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

THANK YOU NOTE

New PictureThe
family of the late Dr. John Edward Mchechu of Ukonga, Dar es salaam
would like to express their heartfelt appreciations to relatives,
colleagues, friends and all those who rendered their moral, spiritual
and material support during treatment, mourning and funeral of their
beloved father Dr. John Edward Mchechu who passed away on 21st July 2015
at his residence in Ukonga and was laid to rest on 26th July 2015 at
MuhezaTanga.
Special thanks are reserved for
the President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Dr.
JakayaMrishoKikwete, The Vice President of the United Republic of
Tanzania, His Excellency Dr. Mohamed Gharib Bilal, the Prime Minister of
the United Republic of Tanzania, His Excellency MizengoPeter Pinda,
Ministers, Members of Parliament, Government Officials and Heads of
Institutions for their moral support extended to us during his illness
and demise.
Also, we would like to extend our
special thanks to Employees and NHC Board of Directors, Serengeti
Breweries, KCB, DAWASCO, Rafiki Club, Soul Sistaz, New Millennium Women
Group, Beach Ladies, Sistaz Club, Doctors and nurses of Muhimbili, Hindu
Mandal, Apollo Hydrabad hospitals and Arafa Dispensary for their
tireless support and cooperation accorded to us during our difficult
time.


Similarly, our thanks go to Priests of Mbezi Beach Lutheran
Church, Anglican churches of St. Paulo Ukonga and St. Peter Muheza,
prayer groups and choirs from different faith groups for their spiritual
support and services.
Overwhelmed by gestures of
goodwill we find ourselves space-bound to thank everyone individually,
we pray that you kindly accept this note as a token of our sincere
appreciations and deep gratitudes, for consoling us in these most
difficult times of loss of our beloved father.
Requiem Mass

The family of the late Dr. John Edward Mchechu would like to
invite you all to the Requiem Mass that will be held on Saturday 12th
September 2015 from 8:00 am at St. Peter Anglican Church Mkuzi, Tanga.
You are all welcome.
Eternal rest grant unto him O’lord and let perpetual light shine upon him, may his soul rest in peace. Amen!
MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU

A SAFE AND FUN HAVEN FOR FAMILIES

IMG_7896


Head of Marketing The Walt Disney Company Africa, Deirdre
King, talking to journalists (not in picture) who were attending
the second edition of MultiChoice Africa Content Showcase
Extravaganza #OnlyTheBest which held in Outrigger Mauritius Beach
Resort, Bel Ombre recently.



(Photo by Zainul Mzige of Modewjiblog)


…………………………………….


Disney Junior, which airs on DStv channel 309 and GOtv Plus
channel 60, is learning-focused and reflects the emotional connection
that generations of consumers have to Disney storytelling and
characters, both classic and contemporary. It invites mum and dad to
join their child in the Disney experience of magical, musical and
heartfelt stories and characters, while incorporating specific learning
and developmental themes.



Reaching over 1.3 million kids and their families across
Africa every day, Disney Junior now airs in 111 countries, with 9 visual
feeds in 16 languages, representing a total of 47 million households
across EMEA.



Launched in June 2011 in Africa, Disney Junior is the
multiplatform entry point to all things Disney, starting from
preschoolers ranging up to 7 year olds, and their carers and parents.
With creative storytelling and engaging characters we help make learning
a playful experience, whilst ensuring that parent and caregivers can
immerse their kids in a safe and fun environment.



Highlights across the Disney Junior channel includes:


Disney Junior’s animated television series, Sofia the First,
is set in the storybook world of Enchancia. It tells the story of
Princess Sofia – an adventurous little girl who is learning how to
adjust to royal life after her mother marries the king and she becomes a
princess overnight. Sofia is learning how to adjust to life with her
new family which includes her step-father, King Roland II, and
step-siblings Amber and James. Along the way, this ordinary girl learns
to navigate the extraordinary life of royalty, and in the process makes
everyone around her feel special.



Showcasing the hallmarks of great Disney storytelling,
fantasy and wish fulfilment, Disney Junior’s animated series, Doc
McStuffins, tells the story of a nurturing six-year-old girl who can
talk to the stuffed animals and toys that she cares for in her playhouse
clinic. When Doc puts on her stethoscope, something magical happens;
toys, dolls and stuffed animals come to life and she can communicate
with all of them, including the toys belonging to her friends and other
neighbourhood children.



Not only a ratings hit, the show has sparked a cultural nerve
in the U.S., generating applause on parent blogs, Facebook and even in
academia for its positive vocational message for African-American girls.
Viewer Dr. Myiesha Taylor, who watches the show with her four year-old,
was moved to create an online collage featuring an image of Doc,
encircled by photos of 131 black women who are Doc’s real life
counterparts. “We are trailblazers,” Taylor proclaimed on her website.
“We are women of colour. We are physicians. We ARE role-models. We
are Doc McStuffins all grown up!”



Disney Junior’s Annie Award-winning series, Jake and the
Never Land Pirates, is a music-filled interactive treasure hunt that
introduces a crew of kid pirates – leader Jake and pals Izzy and Cubby –
and follows their Never Land adventures as they work to outwit two
infamous characters, the one and only Captain Hook and Mr. Smee, from
Disney’s classic, Peter Pan.



Minnie, Goofy, Donald, Pluto and Daisy all join Mickey
in Mickey Mouse Clubhouse, Disney Junior’s vibrant interactive series
that invites young viewers to help solve challenges and overcome
obstacles. Each engaging story features a different theme and offers
cognitive, social and creative-learning opportunities through a dynamic,
play-along experience. Interactivity is key from start to finish as
Mickey speaks directly to preschoolers, asking questions and encouraging
them to play games, participate in special phrases or cheers, and solve
puzzles to reach a goal.



Together with heritage animated series such as Gummi
Bears, Chip ‘n Dale, Ducktales and classic Disney
movies Aladdin, Cinderella and more, Disney Junior continues to create
shared Disney memories between young and old viewers alike.



As of 1 October 2015,
Disney Africa will launch the Disney Junior Africa Facebook page,
giving parents and caregivers their very own Disney Junior experience on
social media.



For more information, please visit 



shukrani

New PictureFamiliayamarehemuDr.
John Edward Mchechu wa Ukonga Dar es salaam wanapenda kutoa shukrani
zao za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nao na
kuwafariji kwa hali na mali katika kumuuguza na mpaka kumlaza katika
nyumba ya milele mpendwa baba yao Dr. John Edward Mchechu aliyefariki
tarehe 21/07/2015 nyumbani kwake Ukonga na kuzikwa tarehe 26/07/2015
Muheza, Tanga.
Shukrani za pekee zimfikie Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
JakayaMrishoKikwete,MakamuwaRais,Dk. Mohamed Gharib Bilal, WaziriMkuu,
Mh. Mizengo Peter Pinda, Mawaziri, Wabunge,
WakuuwaMashirikanaWafanyakaziwaSerikalikwakutufarijikipindichote cha
kuumwa kwake mpaka alipotwaliwa kutoka ulimwengu huu.
Shukrani za pekee pia ziwafikie
wafanyakazi na wajumbe wa bodi ya NHC, Serengeti Breweries, DAWASCO,
KCB, Rafiki Club, Soul Sisters, New Millenium Women Group, Beach Ladies,
Sisters Club, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Muhimbili, Hindu
Mandal, Apollo Hydrabadna Dispensary yaArafa.
Mapadri na wachungaji wa kanisa la
Kiinjili la Kilutheri la Mbezi Beach, Makanisa ya Anglikana ya
Mtakatifu Paulo la Ukonga, Dar es Salaam na Mtakatifu Petro la
Mkuzi,Tanga, kwaya mbalimbali na vikundi vya maombi kwa msaada wao wa
kiroho.
Tunawakushukuru mtu mmoja mmoja
lakini haiwezekani kwani watu ni wengi sana, tunaomba tu mpokee shukrani
zetu za dhati kutoka moyoni mwetu kwajinsi mlivyotufariji katika
kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu.
Misa ya Shukrani

Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wanapenda
kuwakaribisha wote katika misa ya shukrani itakayofanyika siku ya
Jumamosi tarehe 12/09/2015 kuanzia saa mbili asubuhi katika kanisa la
Mtakatifu Petro Mkuzi, Tanga. Karibuni sana mjumuike nasi.
Raha ya milele umpeeeh Bwana wamilele umwangazie apumzike kwa amani, Amina
MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU.

UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA

 Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu kampuni hiyo  kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya
pamba,kama chanzo cha nishati ya umeme kinachotumika kuendeshea
mitambo.Kushoto ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday
Kidolezi.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya
Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond, akizungumzia mradi wa matumizi ya
mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,ambacho ni chanzo cha nishati ya
kuendesha mitambo kiwandani hapo.Nishati ni rafiki wa mazingira  kwa
sababu haina hewa ukaa.Wanaokoa Dola za Kimarekani (USD) 400,000 hadi
500,000 kwa mwaka ambazo zingetumika kununua mafuta mazito na dizeli ya
kuendeshea mitambo .
Waandishi wa habari wakiongozwa na
 Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond(wa
kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo unaotumia mapumba ya mchele
na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya umeme inyotumika kuendesha
mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa TBL,
Sunday Kidolezi.
Meneja wa Nishati na Maji wa
Kampuni ya Bia (TBL)Mwanza, Sunday Kidolezi (wa kwanza kulia),wakiwa na
waandishi wa habari wakati wakitembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa
kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.wa Kwanza kutoka kushoto
(mwenye shati jeupe), Ni Meneja wa Kiwanda hicho, Raymond Richmond.
Meneja wa Kampuni ya Bia (TBL)
Mwanza,Raymond Richmond (mwenye shati jeupe) akiwaonesha waandishi wa
habari mtambo unaozalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba ya mchele
na mashudu ya pamba kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kiwanda
hicho.anaoshuhudia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo,Sunday
Kidolezi (mwenye fulana ya mistari).Mwingine ni mwandishi wa habari wa
kampuni ya The Guardian, Daniel Mkate,ambaye ni miongoni mwa  waandishi
wa habari waliotembelea kiwanda hicho.
Raymond Richmond, Meneja wa
kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo
pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha nishati ya umeme wa
kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa
kampuni hiyo.
Mwandishi wa habari, Daniel Mkate
(kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa  Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,
Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday
Kidolezi, kuhusu  changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na
madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni
ya Bi (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba kwenye magunia, kabla ya kuingizwa
kwenye mtambo wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.Hapo ni katika eneo
 linalotumika kupakulia shehena ya mapumba hayo ya mchele, kutoka kwa
msambazaji.
Meneja wa kiwanda cha Kampuni ya
Bia (TBL) Mwanza,Raymond Richmod, akiwaonyesha waandishi wa habari,
Daniel Mkate wa TRhe Guardian (nyuma) na Henry Kavirondo wa Chanel
Ten,mashine inayosukuma mapumba ya mchele na mashudu ya pamba, kwenda
kwenye mtambo wa kufua umeme unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda
hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday
Kidolezi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kampuni
ya Bia (TBL) Mwanza,wakijaza mapumba ya mchele kwenye mashine kwa ajili
ya kuyasukuma kadi kwenye mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme,
unaotumiwa kuendesha mitambo ya uzalishaji ya kiwanda hicho.
Meneja wa Maji na Nishati wa
kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati
ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa
kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni
Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.

MAPOKEZI YA DR JOHN POMBE MAGUFULI JIJINI TANGA




Bi. Samia Suluhu Ahaidi Umeme Kila Kijiji Ruvuma, Viwanda vya Mahindi, Kahawa


Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, 
Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.
MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake
mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa
wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.
Bi. Samia Suluhu ambaye
amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani
Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake
amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha
inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea
maendeleo ya wananchi.
Alisema kwa kuwa mkoa huo
unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha
viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na
kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa
ambapo wamekuwa wakilanguliwa.
Alisema viwanda vingine ambavyo
Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na
kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya
kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea
uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia miundombinu ya
barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema
serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli
pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo
hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.
Hata hivyo kiongozi huyo amesema
Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,
2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na
rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha
nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama
kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.
Ziara ya mikutano ya kampeni ya
mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa
wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama
hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na
kuunda dola.
Pichani
juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja
cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa
urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
 
 
Pichani
juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja
cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa
urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu. 
 
 
Pichani
juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea
mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia
Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara
ukiendelea. 
Mmoja
wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama
akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha
Maguu, Wilaya ya Mbinga. 
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma,
Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa
kampeni.  
 
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni
wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria
mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha
kijana huyo. 
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Sherehe za Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki Kwa Rais Kikwete Ikulu

unnamed
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo
amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi
ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala
Uganda.
Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo
Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla
fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Septemba 8, 2015 .
asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo Rais kikwete amepokea tuzo ya kuitambua
Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na
Utulivu,Huduma bora za jamii,na maendeleo makubwa ya kiuchumi katika
kipindi cha miaka kumi.
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisaini kumbukumbu maalum ya taasisi ya East Africa Books of Records
mara baada ya kupokea tuzo maalum ya kiongozi bora Afrika mashariki kwa
kudumisha amani nchini na katika jumuiya ya


Afrika Mashariki kwa ujumla hususani Kenya baada ya uchaguzu
mkuu na Burundi hivi karibuni.Kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Africa Book of Records Dkt.Paul Bamutize na kulia ni Mkuu wa
kitengo cha utafiti katika taasisi hiyo Bwana Luzindana Adam Buyinza
.
4
Rais Dkt.Jakaya Mrisho akitoa hotuba yake baada ya kupokea Tuzo ya Kingozi bora Afrika Mashariki.
3
Mwakiulkishi kutoka ubalozi wa
Uganda nchini Tanzania Bwana Stephen Kiyingi akitoa hotuba yake na
ushuhuda jinsi Tanzania ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika miaka
kumi iliyopita.
2
Baadhi ya Wageni walihudhuria hafla hiyo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
7
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza mabalozi kutoka nchi za Afrika ya Mashariki muda mfupi baada ya kupokea Tuzo.
6
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, mabalozi kutoka nchi za
Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tassisi ya
East Africa Book of Records ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  5
Wataalamu wa Utafiti kutoka
Taasisi ya East Africa Book Of Records wakiwa katika picha ya pamoja na
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada kutunikiwa Tuzo
hiyo.Kutoka kjushoto ni Kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul
Bamutize,Watatu kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utafili cha taasisi hiyo
Bwana Luzindana Adam Buyinza na kulia ni Afisa mwandamizi wa Taasisi
hiyo Bwana Kato Issa.
(Picha zote na Freddy Maro)

Rais Kikwete apokea ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

 unnamedx
Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa
India Narendra Modi ambaye pia ni Waziri wa nchi anayeshughulikia
Maendeleo ya Ujasiriamali Mhe.Shri Rajiv Pratap Rudy akiwasilisha kwa
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete barua yenye ujumbe kutoka kwa kiongozi
huyo wa India ikulu jijini Dar es Salaam Septemba 8, 2015 .
c
Rais Dkt.Jakaya Mrisjo Kikwete
akisoma barua yenye ujumbe kutoka kwa waziri Mkuu wa India mara baada ya
kukabidhiwa ikulu jijini dar es Salaam Septemba 8, 2015

(Picha na Freddy Maro)

shukrani

New PictureFamiliayamarehemuDr.
John Edward Mchechu wa Ukonga Dar es salaam wanapenda kutoa shukrani
zao za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nao na
kuwafariji kwa hali na mali katika kumuuguza na mpaka kumlaza katika
nyumba ya milele mpendwa baba yao Dr. John Edward Mchechu aliyefariki
tarehe 21/07/2015 nyumbani kwake Ukonga na kuzikwa tarehe 26/07/2015
Muheza, Tanga.
Shukrani za pekee zimfikie Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
JakayaMrishoKikwete,MakamuwaRais,Dk. Mohamed Gharib Bilal, WaziriMkuu,
Mh. Mizengo Peter Pinda, Mawaziri, Wabunge,
WakuuwaMashirikanaWafanyakaziwaSerikalikwakutufarijikipindichote cha
kuumwa kwake mpaka alipotwaliwa kutoka ulimwengu huu.
Shukrani za pekee pia ziwafikie
wafanyakazi na wajumbe wa bodi ya NHC, Serengeti Breweries, DAWASCO,
KCB, Rafiki Club, Soul Sisters, New Millenium Women Group, Beach Ladies,
Sisters Club, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Muhimbili, Hindu
Mandal, Apollo Hydrabadna Dispensary yaArafa.
Mapadri na wachungaji wa kanisa la
Kiinjili la Kilutheri la Mbezi Beach, Makanisa ya Anglikana ya
Mtakatifu Paulo la Ukonga, Dar es Salaam na Mtakatifu Petro la
Mkuzi,Tanga, kwaya mbalimbali na vikundi vya maombi kwa msaada wao wa
kiroho.
Tunawakushukuru mtu mmoja mmoja
lakini haiwezekani kwani watu ni wengi sana, tunaomba tu mpokee shukrani
zetu za dhati kutoka moyoni mwetu kwajinsi mlivyotufariji katika
kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu.
Misa ya Shukrani

Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wanapenda
kuwakaribisha wote katika misa ya shukrani itakayofanyika siku ya
Jumamosi tarehe 12/09/2015 kuanzia saa mbili asubuhi katika kanisa la
Mtakatifu Petro Mkuzi, Tanga. Karibuni sana mjumuike nasi.
Raha ya milele umpeeeh Bwana wamilele umwangazie apumzike kwa amani, Amina
MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU.

DR. JOHN POMBE MAGUFULI ALITIKISA JIJI LA TANGA, WANANCHI WAFURIKA VIWANJA VYA TANGAMANO KUMSIKILIZA

1


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja
vya Tangamano mjini Tanga leo, Dr. Magufuli amewaomba wananchi wa Tanga
kumpigia kura za ndiyo ili aweze kufanya kazi na kulitumikia taifa,
yeye kwake ni Kazi tu! kwani hata biblia inasema “Asiyefanya kazi na
asile”.
Ameongeza kwamba mara
atakapochaguliwa na kuongoza nchi ya Tanzania atahakikisha anafufua
viwanda mbalimbali vilivyopo nchini na kujenga viwanda vipya
vidogovidogo, vya kati na vikubwa ili kupunguza tatizo la ajira nchini
lakini pia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla wake, Huku akiahidi kubana
matumizi hovyo ya fedha za serikali ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa
hali ya chini ambao wanasumbuka na umasiki.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Mwezi Oktoba Mwaka huu nchini
kote ukishirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-TANGA)
2
Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye  mkutano wa kampeni
zake uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga.
3
Mwanamuziki nguli hapa nchini Diamond Platnumz akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano huo wa kampeni.
4
6
Mwanamuziki Ali Kiba akionyesha uwezo wake katika jukwaa wakati akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jijini Tanga.
8
Mzee Yusuf Makamba akizungumza
neno katika mkutano huo na kuwafunda wananchi wa mkoa huo kutopoteza
kura yao na kumpa Dr. John Pombe Magufuli wa CCM ili awatumikie.
9
Tangamano ikiwa imetapika umati wa wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli.
10
Yamoto Band wakitifua jukwaa.
12
Mwanamuziki wa muziki wa taarab Mzee Yusuf naye akipagawisha wananchi katika mkutano huo.
13
Kada wa CCM na mwenyekiti wa
Chama cha walemavu Ndugu Amon Mpanju akiwahutubia wananchi na kumpigia
debe Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha
Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
15
Ummy Mwalimu akizunguza jambo katika mkutano huo.
16
Mwigulu Nchemba mgombea ubunge
jimbo la Iramba Magharibi naye akatema cheche na kusema wapinzani ni
watu wa dili tu, kila kitu dili.
17
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli
akimkaribisha Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli mkoani Tanga.
????????????????????????????????????


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akiwapungia mikono wananchi wa mkoa wa Tanga mara baada ya
mkutano kumalizika.
????????????????????????????????????


????????????????????????????????????


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza na mgombea ubunge wa jimbo la
Bumbuli Mh. Januari Makamba kulia ni Mgombea ubunge wa jimbo la Iramba
Magharibi Mwigulu Nchemba.
????????????????????????????????????


????????????????????????????????????


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Pangani
leo.
????????????????????????????????????


Baadhi ya vijana waliokuja
kumsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakifuatilia hotuba yake
huku wakiwa juu ya miti. 
????????????????????????????????????
\
Akina mama wakiwa wamejifunika na
mabango yenye ujumbe wa kampeni ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano
ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli
yanayosema “Magufuli Hapa Kazi Tu” wakiwa katika mkutano wa kampeni
mjini Pangani. 
????????????????????????????????????


Vijana wakiwa katika miti
wakimsikiliza Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati akiwahutubia
wananchi.
????????????????????????????????????


Hapa ni rangi za CCM tu.
????????????????????????????????????


Hii nyumba iliyopo kijiji cha
Mkuza Mheza ni full mchanganyiko wao hawana bifu wanadhihirisha kwamba
siasa siyo uadui kwa kuweka picha za wagombea wa CCM na UKAWA. 
????????????????????????????????????


Mzee huyu na Mgombea Udiwani wake kata ya Mkuza.
????????????????????????????????????


Hawa wanaonekana wamekunwa na
sera za Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama
Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli 
????????????????????????????????????


Hapa wakapaza zaidi sauti zao wakisema “Wewe ni  Tingatinga letuuu!!
????????????????????????????????????


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akimnadi Balozi Adadi Rajabu ambaye anagombea ubunge kupitia
jimbo la Muheza.
????????????????????????????????????


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni mjini Muheza.
????????????????????????????????????


 Dr. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi Adadi Rajabu mgombea ubunge wa jimbo la Muheza.
????????????????????????????????????


Mchezea Chatu wa ngoma za utamaduni naye hakusita kufanya mambo yake katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Muheza.
????????????????????????????????????


Vijana wa Kabuku wakampokea Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????


Mgombea Urais wa jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe
Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkata akiwa njiani kwenda Muheza,
Pangani na Tanga mjini kwa ajili ya mikutano ya Kampeni ambapo
aliwaambia atahakikisha anatatua tatizo la maji Mkata mara
atakapochaguliwakuongoza nchi ya Tanzania.
????????????????????????????????????
Wananchi wakimsikiliza Mgombea
Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM
Dr. John Pombe Magufuli huku kukiwa na madumu kwa ajili ya kuchotea
maji Mkata ina tatizo kubwa la maji safi ya kunywa.

TASWIRA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE KUPITIA VIPODOZI VYA LUV TOUCH MANJANO

  
Mkurugenzi
Mtendaji   8020 Fashion na  Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation
Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa
Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na
Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya
biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.
Washiriki wa Mafunzo hayo  wakisikiliza kwa Makini Mada Mbalimbali zilizokuwa Zikijadiliwa.
 Mafunzo
ya Ujasiriamali kwa Mwanamke wa Kitanzania kwa Kutumia Vipodozi vya
LuvTouch Manjano yanaendelea.Mradi huo ulianzishwa kuwejengea Uwezo
wanawake Kwenye Ujasiriamali yakisimamiwa na Taasisi ya Manjano
Foundation.
 Lengo la Mradi
huo
ni kuona kwamba wanwake hawa wanajisimamia na kujikita vizuri kwenye
Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara zao kwa lengo
la kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za ukosefu wa ajira
kuwa chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu mahitaji yake ya msingi,
yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa kupitia
ujasiriamali.
 Pamoja
na mafunzo ya biashara, washiriki hawa watanufaika na utaalamu
(Proffessional Makeup Artist).Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo
imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo
zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea ugumu wa kipato na
ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha
yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake,
Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha
wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
 Mradi huu Uzinduliwa mwezi Mei mwaka huu na Mama Tunu Pinda. 
Mafunzo
haya yametolewa kwa zaidi ya Wanawake 30 ambapo wengi wao tayari
wameshaanza kunuafaika na kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano ambapo
wamewezeshwa
 
 Washiriki hao wakiwa kwenye Picha ya Pamoja

Rais Kikwete apokea tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki

unnamed
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo
amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi
ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala
Uganda.
Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo
Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla
fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Septemba 8, 2015 .
asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo Rais kikwete amepokea tuzo ya kuitambua
Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na
Utulivu,Huduma bora za jamii,na maendeleo makubwa ya kiuchumi katika
kipindi cha miaka kumi.
(picha na Freddy Maro)

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA KUHUSU MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI AGOSTI, 2015

 Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim
Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi
Agosti, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei,
Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………

Na Dotto Mwaibale
 
UWEZO
wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia
shilingi 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010
ikilinganishwa na shilingi 62 na senti 98 iliyokuwa mwezi Julai, 2015.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim
Kwesigabo wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi
Agosti, 2015 kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.
Kwesigabo
alisema mfumuko wa bei wa mwezi Agosti 2015 unaopimwa kwa kipimo cha
mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na asilimia 0.41
iliyokuwa mwezi Julai, 2015.
“Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 mwezi Agosti, 2015 kutoka 158.78 mwezi Julai, 2015.
 
Alisema
kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei
za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula, baadhi ya bei za bidhaa zisizo za
vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa
asilimia 2.0, mafuta ya taa kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia 1.4,
dizeli kwa asilimia 3.8 na petroli kwa asilimia 8.3.
Gwesigabo
alisema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima
kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinatumiwa
na kaya binafsi.
Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai 2015.
Aliongeza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015.
Alisema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 kwa mwezi Agosti, 2015 kutoka 149.31 mwezi Agosti, 2014.
Alisema
Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti
2015 umepungua hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 10.6 ilivyokuwa mwezi
Julai 2015.
Alisema
mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki mfumuko wa bei
nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrioka
Mashariki ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti 2015 nchini Kenya
umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda
umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA WAGANGA WAKUU WA
MIKOA, HALMASHAURI NA WAKURUGENZI WA HOSPITALI ZA RUFAA, JIJINI DAR ES
SALAAM LEO

X9
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Stephen Kebwe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais kufungua Mkutano huo.
 Picha zote na OMR
X2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati
akifungua rasmi Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri
na Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na
Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye
Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.  
X3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Prof.
Philemon Sarungi, akiwa ni mmoja kati ya Viongozi waliowahi kuiongoza
Wizara ya Afya. Sarungi alikabidhiwa tuzo hiyo , wakati wa hafla ya
ufunguzi wa  Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na
Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na
Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye
Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.   Katikati ni
Naibu Waziri wa Afya, Stephen Kebwe (kushoto) ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Afya, Dkt. Donan Mmbando.
X4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Mhe.
Anna Abdallah, akiwa ni mmoja kati ya Viongozi waliowahi kuiongoza
Wizara ya Afya. Anna alikabidhiwa tuzo hiyo, wakati wa hafla ya ufunguzi
wa  Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na
Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na
Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye
Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.   Katikati ni
Naibu Waziri wa Afya, Stephen Kebwe.
X5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Naibu
Waziri wa Afya, Stephen Kebwe, kwa mchango mkubwa wa kuiongoza Wizara
hiyo. Kebwe alikabidhiwa tuzo hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa
 Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Wakurugenzi
wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na Maadhimisho ya Miaka
40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye Hoteli ya Blue Peal
Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.   Katikati ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Afya, Dkt. Donan Mmbando.
X6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Dkt.
Deo Mtasiwa, kwa mchango mkubwa wa kuiongoza Wizara hiyo akiwa Mganga
Mkuu wa Serikali. Mtasiwa alikabidhiwa tuzo hiyo wakati wa hafla ya
ufunguzi wa  Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na
Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na
Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye
Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.   Katikati ni
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Stephen Kebwe.
X8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti
Prof. Janabi, kutoka Kitengo cha Moyo Muhimbili kwa kutambua mchango
wake akiwa ni miongoni mwa watu walioshiriki Jitihada ya kudhibiti Janga
la Ugonjwa wa Ebola Afrika Mashariki. Janabi alikabidhiwa Cheti hicho
wakati wa hafla ya ufunguzi wa  Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa
Mikoa, Halmashauri na Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo
Sept 8, 2015 na Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo
uliofanyika kwenye Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es
Salaam.   Katikati ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Stephen Kebwe.
X7
Msanii Mrisho Mpoto, na wasanii wa
kundi lake la Mjomba Band, wakiigiza kutoa ujumbe kuhusiana na Siku ya
Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo, wakati wa hafla ya
ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na
Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 kwenye
Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
  X10
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo
kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, wakimsikiliza Makamu wa Rais
wakati akihutubia kufungua rasmi Mkutano huo.
X11
12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Viongozi na washiriki wa mkutano huo mara baada ya
kuufungua.

MABWAWA YA MAJI TAKA ENEO LA VINGUNGUTI

1


Mratibu wa Mradi wa kuzalisha
gesi ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika fani ya Uhandisi wa
Mazingira, Chuo Kikuu cha Ardhi John Rutahirwa Akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari kuhusu moja ya mtambo wa kukusanyia maji taka kutoka
majumbani eneo la mradi wa kuzalisha gesi Vingunguti.Gesi hiyo itaanza
kutumika mwezi Desemba mwaka huu.

4
Mtaalam anayehusika na ujenzi,
mafunzo na usimamizi wa mfumo wa mradi wa kuzalisha Gesi
Vingunguti ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya
Uhandisi wa Mazingira, Chuo Kikuu cha Ardhi Rukia Yange akitoa maelezo
kwa waandishi wa habari kuhusu maji taka yanayokusanywa eneo la
Vingunguti ambayo yatazalisha nishati ya Gesi na kuwahudumia wanaoishi
kuzunguka mabwawa ya Maji Taka Vingunguti.
2
Meneja Uhusiano wa DAWASCO Bi.Neli
Msuya (kulia) akiwa na Mtaalam anayehusika na ujenzi, mafunzo na
usimamizi wa mfumo wa mradi wa kuzalisha Gesi Vingunguti ambaye pia ni
mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya Uhandisi wa Mazingira, Chuo
Kikuu cha Ardhi Rukia Yange wakionyesha moja ya kifungashio cha Gesi
itakayotumika majumbani Kutokana na maji taka yanayokusanywa eneo la
Vingunguti.Mradi huo unalenga kuwapunguzia  wananchi gharama za uhifadhi
wa maji taka na kuwapatia nishati ya gesi kwa gharama nafuu
itakayowasaidia kuondokana na matumizi ya mkaa.
3 
umanne Saidi Fundi ujenzi wa vyoo
na msimamizi wa mradi wa majaribio wa Biogasi Vingunguti akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kazi ya ufungaji wa miundombinu
ya kuzalisha gesi katika eneo la Vingunguti.
5
Mtambo wa kuzalisha Gesi katika
katika eneo la Mradi wa Majaribio eneo la Vingunguti unaokusanya maji
taka moja kwa moja kutoka katika makazi ya wananchi.Mtambo huo kwa
mujibu wa maelezo ya watalaam wa mradi huo una uwezo wa kukaa ardhini
kwa kipindi cha miaka 50.
6
Moja ya choo cha kisasa kilichojengwa katika moja ya familia kwa ajili ya mradi wa kuzalisha Gesi katika eneo la Vingunguti.
7
Eneo la  Mtaa wa mji mpya
Vingunguti ambako mabomba ya kupitishia maji taka kutoka kwenye vyoo vya
wananchi ambayo huenda moja kwa moja kwenye mtambo wa kuzalishia Gesi.
……………………………………………
Na.Aron Msigwa – MAELEZO. Dar es salaam.
Wakazi wa mtaa wa mji mpya, kata
ya Vingunguti, Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wako mbioni
kuanza kunufaika na mradi wa uzalishaji wa Gesi inayotokana na maji taka
ya vyoo vyao na yale ya yaliyo katika mabwawa makubwa ya kuhifadhia
maji taka yaliyo katika eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika eneo unapojengwa mradi wa majaribio wa kuzalisha Gesi,
Mratibu wa Mradi huo ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika fani
ya Uhandisi wa Mazingira, Chuo Kikuu cha Ardhi John Rutahirwa amesema
kuwa wananchi wataanza kutumia gesi itakayozalishwa kuanzia mwezi
Desemba mwaka huu.
Amesema kazi ya kufanikisha
ujenzi wa miundombinu ya mradi huo inaendelea chini ya usimamizi wa
Mamlaka ya Maji Taka (DAWASA) kwa kushirikiana na Wanafunzi wa fani ya
Uhandisi wa Chuo Chuo Kikuu cha Ardhi na Taasisi isiyo ya kiserikali ya
wanafunzi wanaosomea fani ya uhandisi wa Mazingira (CDI) ya Chuo kikuu
cha Cambridge, Uingereza.
Amesema wanafunzi wanaosomea
fani ya Uhandisi wa Mazingira wa Chuo Kikuu cha Cambridge,Uingereza kwa
kushirikiana na baadhi ya wanafunzi wanaosomea Uhandisi wa Mazingira wa
Chuo Kikuu cha Ardhi nchini Tanzania walikuja na wazo na kubuni mradi
huo wenye lengo la kuboresha maisha kupitia maji taka.
Amesema chini ya uratibu wa
DAWASA yenye jukumu la kusimamia miundombinu ya maji taka na Taasisi ya
mikopo la Bridge for change  ya Tanzania inayotoa mikopo midogo midogo
kwa wananchi walianza kufanya mapitio kwa  kila nyumba ili kuona namna
wanavyoweza kutumia changamoto ya maji taka katika eneo hilo kwa
kuigeuza kuwa fursa.
Amefafanua kuwa wakihusisha
wataalm wa mradi na viongozi wa mtaa wa vingnguti mji mpya, walianza
 kuzungumza na kujadiliana na wakazi wa eneo hilo ili kuwezesha kazi ya
 kuunganisha vyoo vyao katika mtandao wa mabomba ya kusafirisha maji
taka kuelekea kwenye mtambo wa kuzalisha gesi.
Amefafanua kuwa  chini ya mradi
huo maji taka yote kutoka kutoka katika  nyumba zilizounganishwa kupitia
mabomba yanakusanywa  na kusafirishwa moja kwa moja  kwenye  mtambo wa
kuzalisha gesi.
Kwa upande wake Mtaalam
anayehusika na ujenzi, mafunzo na usimamizi wa mfumo wa mradi huo ambaye
pia ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya Uhandisi wa Mazingira
Chuo Kikuu cha Ardhi Rukia Yange amesema mradi huo ambao uko kwenye
majaribio unalenga kuwapunguzia  wananchi gharama za uhifadhi wa maji
taka kwa kuwapatia nishati ya gesi kwa gharama nafuu itakayowasaidia
kuondokana na matumizi ya mkaa.
Amesema kwa kuanzia
utawanufaisha  watu 150 wa eneo hilo na kuongeza kuwa kuanzia Desemba
mwaka huu wataanza kuiweka gesi hiyo katika vifungashio maalum
vitakavyoanza kusambazwa majumbani mwao tayari kwa matumizi.
Amesema gesi hiyo itamwezesha
mwananchi kuitumia kwa kipindi cha mwezi mmoja na kupunguza  matumizi
makubwa ya mkaa na uharibifu wa mazingira.
Aidha, amesema gharama za
mwananchi kuunganishwa katika mfumo huo inaanzia shilingi 150,000/ kwa
wale walio na vyoo vinavyoruhusu mfumo huo na  shilingi 700,000/= kwa
mwananchi anayetaka kujengewa choo kipya katika eneo lake la makazi
gharama ambazo hulipwa kidogo kidogo kupitia utaratibu wa mikopo nafuu
ulioanzishwa.
Naye Meneja Uhusiano wa DAWASA
 Bi. Neli Msuya akifafanua kuhusu mradi huo amesema suala la ujenzi wa
miundombinu ya kuchukualia maji taka na matumizi ya gesi itakayozalishwa
litakwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi hao juu ya matumizi
na uhifadhi wa gesi hiyo.
Amefafanua kuwa DAWASA
inaendelea kuendesha mafunzo ya uzingatiaji wa usalama katika matumizi
ya gesi hiyo pamoja na suala la usafi, utunzaji na ulinzi  wa
miundombinu ya kusafirishia maji taka iliyojengwa katika eneo hilo ili
iweze kudumu kwa kipindi kirefu.
Ameeleza kuwa mbali na mradi wa
kuzalisha gesi DAWASCO kwa kushirikiana na wadau wa matumizi ya Nishati
endelevu na uhifadhi wa mazingira inatarajia kuanzisha mradi wa
kuzalisha mbolea itakayotokana na maji taka yaliyohifadhiwa katika eneo
hilo.
“DAWASA tukishirikiana na wadau
mbalimbali tuna mpango wa kuyatumia maji taka haya yaliyohifadhiwa
kuzalisha mbolea itakayotumiwa na wakulima katika shughuli za
kilimo,tunalenga kuibadilisha changamoto hii ya maji taka kuwa fursa
itakayowanufaisha wananchi badala ya kuwa kero kwao” Amesisitiza.
Wakiuzungumzia mradi huo baadhi
ya wakazi wa mtaa wa mji mpya ambao vyoo vyao vimeunganishwa kwenye
mfumo wa kusafirishia maji Taka wamesema mradi huo ni ukombozi katika
maisha yao kwa kuwa umewapatia vyoo bora na kuwaondolea adha na gharama
ya uhifadhi wa maji taka    waliyokuwa wakiipata hapo awali kutokana na
ujenzi holela wa makazi yao.
Wameongeza kuwa mradi huo
umewasaidia katika uhifadhi wa mazingira na kuondoa tatizo la
utiririshaji wa muda mrefu wa maji taka uliosababishwa na uwepo wa
mifumo mibovu ya vyoo vyao.
Wamesema kuwa kutokana na
uimarishaji wa mifumo ya kusafirisha maji uliofanywa na DAWASA kwa
kushirikiana na Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Cambrige (CDI) na Taasisi ya utoaji wa mikopo ya Bridge for
Change  wameondoa hofu waliyokuwa nayo ya kupata magonjwa ya mlipuko
ikiwemo kipindupindu na kutoas wito kwa wananchi  katika maeneo mengine
kujiunga na mradi huo.

NEC YAKEMEA VIKALI UKIUKWAJI WA MAADILI UNAOFANYWA NA VYAMA VYA SIASA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI

indexb
MAADILI YA UCHAGUZI KWA

AJILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI YA MWAKA 2015


(chini ya Kifungu cha 124A cha Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 (sura ya 343) 


Sisi Vyama vya Siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pamoja tumekubaliana
kuwa na uchaguzi huru, wa haki, uwazi, na wa kuaminika. Na kwamba Amani,
Ustawi wa Nchi, Usalama wa Raia, Uhuru wa Vyama vya Siasa na Utii wa
Sheria, Kanuni na taratibu za uchaguzi ndio msingi wa uchaguzi ulio
huru, haki na wenye kuzingatia ushiriki wa makundi yote ya jamii katika
uchaguzi. Tunajipa, na tunakubaliana kuwajibika kuyatekeleza maadili
haya yanayotokana na kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya
mwaka 1985, (sura 343). Tutafanya jitihada za wazi kuhakikisha maadili
haya yanajulikana na kuheshimiwa na wagombea na wanachama wote wa Vyama
vya Siasa.



2.0 Maadili kwa Vyama vya Siasa na Wagombea katika kuendesha shughuli za Siasa wakati wa Kampeni.


2.1 Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea.


  1. (c)  Vyama vya Siasa vifanye mikutano ya Kampeni kwa
    kuzingatia ratiba rasmi iliyoratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi au
    Wasimamizi wa Uchaguzi katika kutangaza sera zao. Aidha, mikutano yote
    itafanyika kati ya saa 2:00 asubuhi na saa 12:00 jioni. Bila kuathiri
    muda ulioelezwa hapo juu, Vyama vya Siasa vinaweza kutumia vipaza sauti
    kuanzia saa1:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku kutoa matangazo ya mikutano
    itakayofuata. 
  1. (k)  Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea au Wafuasi
    wao wahakikishe kuwa majengo wanayotumia kufanya kampeni sio ya ibada au
    sehemu zinazotumiwa kwa ajili ya ibada. Vile vile, Vyama vya Siasa
    vihakikishe kuwa havitumii Viongozi wa dini kupiga kampeni kwa ajili ya
    Vyama vya Siasa au Wagombea wao. 

    1. (f)  Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea wao
      hawaruhusiwi kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo ya kampeni ya
      Vyama vingine vya Siasa na matangazo ya Uchaguzi yanayotolewa na Tume ya
      Taifa ya Uchaguzi. 

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda AKABIDHI MAGARI YA KUBEBA WAGONJWA Wilaya ya Ngorongoro

indexWAZIRI
MKUU  Mizengo Pinda amekabidhi magari mawili ya kubeba wagonjwa yenye
thamani ya sh. milioni 150 kwa uongozi wa Wilaya ya Ngorongoro ili
yapelekwe kwenye kituo cha afya cha Enduleni na hospitali ya Wasso
ambayo inatumika kama hospitali ya wilaya.
Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo
ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Septemba 2013 alipofanya
ziara ya kikazi ya mkoa wa Arusha na kubaini adha ya usafiri iliyokuwa
ikiwapata wakazi wa kata za Wasso na Enduleni zilizoko wilayani
Ngorongoro.
Akizungumza na watumishi wa idara
ya afya na wananchi waliohudhuria makabidhiano hayo leo mchana,
(Jumanne, Septemba 8, 2015), Waziri Mkuu alisema aliyapata magari hayo
kwa wafadhili kutoka Japan na sehemu nyingine ambayo haikuitaja.
“Nikiwa ziarani Japan, Machi mwaka
huu, nilikutana na Watanzania waishio Japan nikawaomba kama wanaweza
kunisaidia gari la wagonjwa hata kama limetumika sababu najua kule
magari yaliyotumika huwa yanakuwa hayajachoka. Watanzania wale
walikubali na kuamua kunisaidia kutekeleza ahadi yangu,” alifafanua
Waziri Mkuu.
Alisema mara baada ya ziara yake,
alipeleka maelekezo ya kupata magari kwa ajili ya Wasso na Enduleni
kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini kutokana na upatikanaji
mgumu wa fedha za bajeti, ombi hilo halikufanikiwa ndipo akaona atafute
njia nyingine ya kuwasaidia wakazi hao.
“Ahadi ya Serikali ya kuwapatia
gari la wagonjwa wakazi wa Wasso na Enduleni bado iko palepale lakini
niliona ni vema wakati wakiendelea kusubiri fedha zipatikane, bora
tutafute njia nyingine ya kuwasaidia kupunguza tatizo la usafiri kwa
wagonjwa linalowakabili wakazi hao,” aliongeza.
Waziri Mkuu alikabidhi funguo za
magari hayo mawili kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Hashim
Mgandilwa pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. John
Kurwa.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Bw. Felix Ntibenda Kijiko na viongozi wengine wa mkoa
wa Arusha na waganga wakuu vituo vya Enduleni na Wasso.

Atosha Kisava, Bulenge walitamani Tamasha la amani

Kisava-1NA MWANDISHI WETU
……………………………..
IKIWA maandalizi ya Tamasha la
Amani yakipamba moto, waimbaji Danny Bulenge na Atosha Kisava wamesema
wanatamani kushiriki katika tamasha hilo kubwa la kihistoria
linalotarajia kufanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na Dira ya Mtanzania
hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, walisema kuwa wanatamani wapate
fursa ya kushiriki katika uimbaji katika tamasha hilo lililoandaliwa na
Kampuni ya Msama Promotions la kuombea amani taifa kuelekea uchaguzi
mkuu.
Waimbaji hao ambao wanatamaba na
nyimbo zao mbalimbali walisema kuwa tamasha hilo ni kubwa kwa taifa
hivyo kama waimbaji wanatamani kuweka mchango wao siku hiyo ya kuliombea
taifa amani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati
ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama,
Alex Msama alithibitisha kupata taarifa za waimbaji hao ambako
wanazifanyia kazi.
Msama alisema waimbaji wengi
wameomba kushiriki tamasha hilo huku akiahidi kuwa kamati inangaalia
uwezekano wa waimbaji wote waliomba wakiwemo chipukizi kupata nafasi ya
kuimba siku hiyo muhimu.
Tamasha hilo litanzia mkoa wa Dar
es Salaam Oktoba 4, Morogoro Oktoba 7, Iringa 9,Mbeya Oktoba 11, Dodoma
Oktoba 14, Shinyanga Oktoba 16 na kumaliziwa na Mwanza Oktoba 18.

ZOEZI LA KUGAWA CHAKULA LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA

1
Wakimbizi kutoka nchini Burundi
walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba shehena ya unga wa
mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoaniKigoma.
2
Byesige Josephat (anayemimina
mafuta) na Hezron Mtangirwa (kushoto), wakimbizi kutoka Burundi
waliohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wakipima mafuta
ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana,baada ya kugawiwa mafuta
na Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia chakula (WFP), ambalo
lina kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
3
Kina mama wa kimbizi toka
Burundi wakipata mgao wao wa unga unaotolewa kwa wakimbizi
wanaohifadhiwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma. Serikali kwakushirikiana na Mashirika ya Kimataifa
imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka Burundi wanapata
chakula cha kutosha kwaajili ya mahitaji yao.
4
Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) wakiwa wamebeba mgao wa chakula.
5
Wakimbizi wakifunga shehena ya mahindi.
6
Sehemu ya shehena ya chakula ukiwepo unga wa mahindi na mafuta ya kupikia ikiwa katika ghala la kuhifadhia chakula.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

Flaviana Matata ateuliwa kuwa Balozi wa hiyari wa Utalii Tanzania.

flavyDr
Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa
kwake huku kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za
wizara hiyoFlaviana matata
Mwanamitindo
wa Kimataifa anaefanyia kazi zake za nchini Marekani Flaviana Matata
amechagulia na Wizara ya Maliasili kuwa Balozi wa Hiyari ‘Good Will
Ambassador’ kwa kipindi cha miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza
vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
Flaviana ambaye juzi alikuwa mmoja
kati ya shuhuda wa kushuhudia wizara ya maliasili na utalii wakizindua
rasmi tangazo litakalokuwa linatangaza vivutio vya Tanzania nje ya anchi
alitawazwa leo hii na katibu mkuu Dr Adelhelm James Meru aliyemkabidhi
kwa niaba ya Waziri , Mheshimiwa Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi
Madam Devota Mdachi akishuhudia.


RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA
MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA




 Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole
majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa
kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha,
akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah
na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na
kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa
wameruhusiwa






 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali
ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi
walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni
katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.






 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa
Morogoro Ndg. Hassan BAntu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia
katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.






 Mmoja
wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini
hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo






 Rais
Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa
kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye
msongamano huo






 Rais
Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora
Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika
msongamano huo






 Rais
Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa
kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye
msongamano huo






 Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi





 “Pole sana….” Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi







 Rais
Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa
wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua
kwa moto






 
Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa
wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika
mguu wakati akicheza kwenye mti






Rais
Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea
kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli
katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana 






Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao





Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa





Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye 





Rais
Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo
kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa
hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa
ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.






Mwishoni
Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na
kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya
mkutano wa kampeni kumalizika.






Rais
Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya
 Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa
msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana.



PICHA NA IKULU



SHERIA MPYA YA MTANDAO MWISHO CHUMBE..?

Logo ya Zanzibar Diaspora Association

(ZADIA)

 ………………………………………
Wanadiaspora wameelezea wasiwasi
wao kuwa sheria mpya ya Makosa Ya Mtandao iliyoanza kufanya kazi tarehe
mosi mwezi huu nchini Tanzania, huenda ikaishia Chumbe, imefahamika.
Hayo yamekuja kwenye kongamano
maalum lililoandaliwa na Jumuiya Ya Wazanzibari Waishio nchini Marekani
(ZADIA) kujadili Sheria Mpya ya Makosa Ya Mtandao na Athari zake
Kisiasa.
Wageni rasmi katika kongamano
hilo lililofanyika kwa njia ya simu walikua ni Mwandishi khabari Bi
Salma Said, na Mwanadiplomasia mstaafu Bw. Muhammed Yussuf Mshamba.
Utata wa Kisheria:
Akizungumza kwenye kongamano
hilo, Bi Salma Said alisema kuwa sheria hii itakuwa na utata kutokana na
jinsi ya mchakato mzima wa kuipitisha ulivyokwenda. “Sheria imepitishwa
kimabavu, kwani wadau wote hawakushirikiswa, pia ilipitishwa wakati
Wabunge wa upinzani wakiwa wametoka Bungeni” alifafanua Bi Salma na
kuongeza kuwa Baraza la Wahariri Tanzania liliikataa sheria hiyo na
kupitisha azimio la kumshauri rais Kikwete asiitie saini, lakini
Mheshimiwa rais aliitia saini.
Kwa upande wake, Bwana Muhammed
Yussuf Mshamba ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
alielezea wasiwasi wake juu ya uwezekano wa sheria hiyo kutekelezeka kwa
vile mfumo uliotumika kuiptisha haukukidhi haja.
Akizungumza katika kongamano
hilo, Bwana Mshamba ambaye aliwahi kuwa mtia nia wa kuwania urais wa
Zanzibar kwa tiketi ya CCM alisema “Sharia ile ilipitishwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini Zanzibar hawakupata nafasi ya
kuiangalia”.
“Kwa mujibu wa kifungu cha 234
cha Katiba ya Zanzibar, sharia zote zinazopitishwa na Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na ambazo zinatakiwa kutumika Zanzibar na Bara,
kwa mujibu wa kipengele kile ni lazima Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
lipewe nafasi ya kuziangalia”. 
Alisema Bwana Mshamba na
kuongeza kuwa, sheria ile ilipitishwa wakati Baraza la Wawakilishi
limeshavunjwa na hakukuwa na njia ya kuliitisha angalau kwa kikao cha
dharura ili kuweza kuijadili.
 

NGOMA AFRICA BAND AKA FFU-UGHAIBUNI WAFUNGA KAZI VECHELDE FESTIVAL,UJERUMANI

1
Gwaride la Ngoma Africa jukwaani nyara za taifa chini ya ulinzi wa makamanda.
2
Kikosi Kazi Ngoma Africa Band kazini Vechelde festival-Ujermani.
…………………………..
Kikosi Kazi Ngoma Africa Band
aka FFU-Ughaibuni chenye maskani nchini ujerumani juzi siku ya Jumamosi
ya 5 September 2015 kilifanikiwa kufunika katika
onyesho Vechelde Festival nchini
Ujerumani.bendi hiyo maarufu barani ulaya kwa kuwadatisha washabiki wa
muziki wa kiafrika kule ughaibuni imejijenga umaarufu katika kila kona
na kuwekwa kileleni katika nafasi ya juu na washabiki wake wa
kimataifa.inaongozwa na kamanda Ras Makunja na kuwa na utajiri wa wanamuziki vijana wenye wingi wa vipaji .

DR.JOHN POMBE MAGUFULI: WANA HANDENI NIPENI KURA NIMALIZIE MIRADI YA BARABARA NILIYOKWISHA IANZA

????????????????????????????????????


mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye
uwanja wa CCM wa Kigoda mjini Handeni na kuhudhuriwa na maelfu ya
wananchi wilayani humo, Dr Magufuli amewaomba wananchi wa Handeni
kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu ili Rais na  aweze
kuleta maendeleo na kakamilisha miradi mbalimbali ya barabara aliyoanza
kuitekeleza wilayani humo akiwa Waziri wa Ujenzi.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
na waangalizi wa kimataifa kutoa tamko kufuatia baadhi ya wagombea
kuanza kufanya kampeni chafu wakiingia makanisani na kujinadi na kuomba
kura makanisani jambo ambalo sio jema kwa taifa letu kwani siasa
haihusiani na masuala ya dini.(PICHA NA JOHN BUKUKU
– FULLSHANGWE-HANDENI)
????????????????????????????????????


mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati
akiwahutubia wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kigoda mjini Handeni.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akipanda jukwaani kwenye
mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kigoda Handeni.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wazee wa wilayani Kilindi wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya  Songe Kilindi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kilindi.
????????????????????????????????????
Kada wa CCM Ndugu Amon Mpanju akizungumza na wana Kilindi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Songe.
????????????????????????????????????
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Ndugu Abdallah Bulembo akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mzee Yusuf Makamba akiwahutubia wananchi wa kata ya Songe wilayani Kilindi wakati akimnadi Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Tanga Hery Shekifu katikati nanyekiti wa Wazazi  Ndugu
Abdallah Bulembo wananchi wa Kilindi.
????????????????????????????????????
Baadhi ya Akina mama wa wanachama wa CCM wakiimba huku wakiwa wameshika mabango yene picha ya Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya vijana wakimpungia
mkono Dr. John Pombe Magufuliwakati akiwa njiani kuelekea wilaya ya
Kilindi akitokea mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Akina mama wakimpungia mkono Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi njiani akitokea mkoani Morogoro kwenda Handeni Mkoani Tanga.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Hapa Kazi Tu!
????????????????????????????????????
Lazima tumuone Magufuli
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa wameshika mabango yenye picha ya Sadiq Muradi Mgombea ubunge wa jimbo la Mvomero.
????????????????????????????????????
Mmoja wa wananchi waliohudhuria
katika mkutano wa kampeni mjini Turiani akipata tunda la Chungwa huku
akiwa amekumbatia picha yake yenye picha ya Mgombea wa jimbo la Mvomero
Ndugu Sadiq Murad.
????????????????????????????????????
Wananchi wakiwa na picha za Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika Turiani mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mjini Turiani.
????????????????????????????????????
Kutoka kulia ni Mzee Yusuf
Makamba, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Ndugu Innocent Kalogeres na
Ndugu Sadiq Murad mgombea ubunge jimbo la Mvomero.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mvomero Ndugu Sadiq Murad.
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akisoma moja ya mabango ambayo yaliandikwa na vijana wachoma mahindi wa Dumila. 
????????????????????????????????????
Dr. John Pombe Magufuli akiwasili
katika eneo la Dumila akiwa njiani kuelekea mkoa wa Tanga kupitia
Kilindi, Handeni mkoani Tanga.

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATAJA VYAMA VYA SIASA VYENYE USAJILI WA KUDUMU AMBAVYO VINASTAHILI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Nchini, Monica Laurent (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati
akimkaribisha msemaji wa mkutano huo kuzungumza na waandishi.
Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo
ninastahili kushiriki uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu, Emmanuel Kayuni. 
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo kwenye mkutano huo.

NEC YATOA ONYO KALI DHIDI YA UKIUKWAJI WA MAADILI KIPINDI HIKI CHA KAMPENI

Microsoft Word - TAARIFA KWA UMMA.pdf_page_1

Kama mnavyofahamu Kampeni za
Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani zimeanza tangu tarehe 22
Agosti, 2015 na zinaendelea hadi tarehe 24 Oktoba, 2015.


Ni jambo linaloeleweka kwamba
mchakato wa Kampeni na wa Upigaji Kura unatawaliwa au kuongozwa na
Sheria, Katiba na Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya
mwaka 2015.


Katika kipindi hiki tangu Kampeni
zianze, nafurahi kusema kwa niaba ya Tume kuwa kwa ujumla, Kampeni
zimeenda vizuri. Karibu mikutano yote imefanyika katika hali ya utulivu
na amani. Hatujapata taarifa ya mkutano wa Kampeni ambao umevurugwa kwa
fujo zozote. Kwa hilo napongeza Vyama vyote vya Siasa.


Hata hivyo, kutokana na mikutano
hiyo nchini ya Kampeni, ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani yamejitokeza
mambo ambayo ni kinyume kabisa na Mwongozo wa Maadili ya Uchaguzi wa
Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 uliotiwa saini na Vyama vyote vya
Siasa tarehe 27 Julai, 2015.


Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yamejitokeza katika Kampeni hizo:-

(i) Kutozingatia muda wa kumaliza Mikutano ya Kampeni

Kuna baadhi ya Vyama ambavyo
katika mikutano yao vimekiuka Kipengele hiki kwa kufanya mikutano zaidi
ya saa 12.00 jioni. Kuendelea kufanya Mkutano wa Kampeni zaidi ya muda
huo ni ukiukwaji wa Kipengele cha 2.1 (c) cha Maadili ya Uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 kinafafanua kuwa Mikutano yote
ya Kampeni itafanyika kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.


(ii) Kubandika mabango ya Kampeni, matangazo au Mchoro wowote kwenye maeneo yasiyoruhusiwa au bila idhini ya wahusika

Baadhi ya Vyama vimeanza kubandika
mabango, michoro na picha za Wagombea wao katika majengo au vyombo vya
usafiri vya watu binafsi au Taasisi mbalimbali bila idhini ya wamiliki
husika.


Napenda kuwakumbusha kuwa, kwa
mujibu wa Kipengele cha 2.2. (g) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, hairuhusiwi kufanya hayo bila idhini
ya wamiliki husika.


(iii) Kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo au picha za Kampeni za Vyama vingine

Tume imeanza kupokea malalamiko
kutoka baadhi ya Vyama kuwa, mabango au picha za Kampeni za Vyama vyao
yanabanduliwa au kuchafuliwa na wafuasi wa Vyama vingine.


Ni vema Vyama vya Siasa na
Wagombea wakumbuke kuwa Kipengele cha 2.2 (f) cha Maadili ya Uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, kinapiga marufuku Chama
kingine kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo au picha za Kampeni za
Vyama vingine.


(iv) Matumizi ya lugha zisizo za staha

Tume imepokea malalamiko kuwa,
katika Mikutano mbalimbali ya Kampeni katika ngazi zote, kumeanza
kujitokeza baadhi ya viongozi wa Vyama, Wagombea au wafuasi wao kutumia
lugha zisizo za staha wakati wa Mikutano ya Kampeni katika ngazi
mbalimbali.


Lugha zisizo za staha zinajumuisha
matusi, kejeli, kashfa n.k. Kipengele cha 2.2 (b) cha Maadili ya
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, kinakataza Viongozi
wa Vyama vya Siasa na Wagombea wao kutumia lugha zisizo za staha katika
harakati zote za Kampeni hadi upigaji Kura.


Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea

Viongozi wa Vyama vya Siasa na
Wagombea wana wajibu wa Kisheria wa kuyaheshimu, kuyasimamia na
kuyatekeleza Maadili hayo kwa mujibu wa Kipengele cha 2.1. (b) cha
Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015. Viongozi
wa Vyama vya Siasa na Wagombea wana jukumu la kuwaelimisha,
kuwahamasisha na kuwasisitiza wanachama wao kutekeleza Sheria ya
Uchaguzi (ikumbukwe kuwa Maadili ya Uchaguzi yametungwa chini ya Kifungu
cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343)


Adhabu za ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi

Napenda kuwakumbusha Vyama vya
Siasa na Wagombea kuwa, ukiukwaji wa aina yoyote wa Maadili unaweza
kusababisha Chama au mgombea kupewa adhabu kama zilivyoainishwa katika
Kipengele cha 5.10 (a-f). Adhabu hizo ni pamoja na:


1. Chama au Mgombea aliyekiuka maadili kuelekezwa kuomba msamaha hadharani.

2. Kupewa onyo au karipio.

3. Kumtangaza kupitia vyombo mbalimbali vya habari na taarifa kwa Umma mgombea au Chama kilichokiuka Maadili.

4. Chama au Mgombea kusimamishwa kuendelea kufanya Kampeni.

5. Chama au Mgombea kuzuiliwa kutumia vyombo vya habari.

6. Chama au Mgombea kulipa faini kuanzia kiwango cha 100,000/- 500,000/- na 1,000,000/- kutegemea ngazi ya Kamati husika.

Katika kipindi hiki cha Kampeni,
Chama au Mgombea akipewa mojawapo ya adhabu hiyo kunaweza kuathiri
Kampeni zake za kuelekea Uchaguzi wa Rais, Wabunge au Madiwani.


Hitimisho.

Napenda kunukuu Kipengele cha 1.4
cha Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015
ili kila Chama kione umuhimu wa kuwahimiza wagombea na wanachama wao
kuzingatia Maadili katika harakati zao za kujinadi. Nanukuu:


“[……] kila mgombea atajaza Fomu
Na. 10 kuthibitisha kuwa ataheshimu na kutekeleza Maadili ya Uchaguzi.
[….] Mgombea atakayekataa kusaini Maadili haya atakataliwa au kuondolewa
kushiriki katika Uchaguzi kama Mgombea.”


Maana yake ni kwamba kila Chama,
Mgombea na Wanachama kwa ujumla wana wajibu kuheshimu taratibu zote za
Kampeni hadi kupiga Kura.


Yote yaliyokatazwa katika Maadili
yazingatiwe na Vyama vyote. Kama nilivyosema hapo awali Tume imepata
malalamiko kuwa baadhi ya Vyama na Wagombea wamekiuka Maadili ama kwa
kuzidisha muda wa Kampeni, au kuchana na kuharibu mabango, au kutumia
lugha chafu isiyo na staha; Haya yote Tume inakemea kwa nguvu sana na
kusihi Vyama vyote na Wanachama wao wote kuheshimiana, waeleze sera zao
bila kukashifiana.


Lengo na matumaini ya Tume ni kuwa
na Kampeni za utulivu na hatimaye wananchi kuwa na hali ya utulivu na
amani ili Uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu. Kwenye hali ya utulivu
na amani wananchi wataweza kupiga Kura ya utulivu ili kuamua viongozi
wanaowataka. Hiyo ndiyo Demokrasia.


Nimalizie kwa kuwakumbusha Vyama
vyote kuzingatia Maadili ya 2015. Tume isilazimishwe kuchukua hatua za
kutoaadhabu kwa Vyama na Wagombea. Busara itumike katika mikutano yote
ya Kampeni.


Inawezekana, wote tukidhamiria, “Play your Part”.
Jaji (Mst.) Damian Z. Lubuva

MWENYEKITI

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

IDADI YA MAUZO YA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM YASHUKA


IDADI ya mauzo katika soko la hisa
la Dar es salaam (DSE) imeshuka kwa asilimia 78 kutoka Tsh. Bilioni
29.8 hadi Tsh. Bilioni 6.4 kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.


Aidha idadi ya hisa zilizouzwa katika soko hilo pia zimeshuka
kwa asilimia 60 kutoka Tsh. Milioni11.2 hadi kufikia Tsh. Milioni 4.3
kutokana na makampuni mengi kutowekeza katika soko la hisa.


Akizungumza na waaandishi wa habari leo (Jumatatu Septemba 07,
2015) Meneja Miradi na Biashara wa DSE, Patrick Mususa alisema kuwa hata
hivyo idadi ya mtaji katika soko umekuwa kutoka tilioni 21.8 hadi
tilioni 21.9 ikiwa ni pamoja na ongezeko la idadi ya mtaji wa makampuni
ya ndani kutoka Tsh. Trilioni 9.7 hadi Tsh. Trilioni 9.9.


Aidha Bw.Mususa ameitaja benki ya CRDB kuwa ndiyo inayoongoza
kuuza hisa zake katika soko hilo ikiwa na asilimia 91, ikifuatiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ikiwa na asilimia 7 na Benki ya NMB ikiwa
na asilimia 0.5.


Kwa mujibu wa Mususa alisema kampuni ambazo zinaongoza kwa
ongezeko la bei katika soko la hisa kuwa ni Uchumi Super Market ikiwa na
asilimia 5.5 ikifuatiwa na Benki ya KCB ikiwa na asilimia 4.4 pamoja na
benki ya NMB 3.5


“Viashiria vya soko katika huduma za kibenki vimeongezeka kwa
alama 62, hisa za benki ya NMB zimeongezeka kwa pointi 3.5 ikifuatiwa na
sekta ya viwanda kwa alama 20 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za
TBL”


Mususa alifafanua kuwa pamoja na viashiria vya kibiashara
kushuka kwa alama 4 kulikochangiwa na punguzo la bei ya hisa za
swissport kwa asilimia 0.13, kwa ujumla kiashilia cha soko kimeongezeka.


“DSE tumeboresha huduma zetu kwa kuanzisha huduma ya kimtandao
ya DSE mobile Trading ili kuwawezesha watumiaji wa huduma hizo kujiunga ,
kununua na kuuza hisa kupitia simu ya mkononi