Thursday, May 25, 2017

CCM WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA DHIDI MAUAJI MKOA WA PWANI














 
                                     Na Ismail Mang'ola



            Chama
Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya
Mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkutanga na Rufiji Mkoani Pwani
ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.
        
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, HUMPHEY POLEPOLE, amesema hayo Jijini Dar es
salaam   leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji
yanayoendelea katika Wilaya hizo.
        
POLEPOLE pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza
akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa maujia hayo yanasababisha kuzorota
kwa shughuli za maendeleo.
        
Amesema chama kwa muda mrefu kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa
kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa
sasa imetosha.
Kuhusu suala la uchaguzi
ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema mauaji hayo yanakiweka Chama katika
mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake hivyo ni vema hatua zikachukuliwa
sasa.
        
Katika hatua nyingine, POLEPOLE amesema Chama kimeipongeza Kamati Maalum ya
kuchunguza Mchanga wa Madini kwa kazi nzuri iliyofanywa sanjari na kuwaomba
wananchi kumuunga mkono Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua alizozichukua kwa
watendaji kutokana na