Friday, May 5, 2017

 
DAWASCO inatambua na kuthamini sana
juhudi zinazofanywa na wadau wote wa
huduma zinazotolewa na Shirika tukiamiani
kuwa tunaweka nguvu za pamoja zinazolenga
kukabiliana na changamoto kubwa za
kiuendeshaji na kiuwekezaji kwa lengo la
kuboresha huduma ya maji safi na uondoshaji
wa majitaka jijini Dar es Salaam na miji ya Kibaha
na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Miongoni mwa changamoto za kiuwekezaji
ambazo zimekuwa zikikwamisha huduma ya
maji katika maeneo yanayopata huduma kutoka
DAWASCO ni pamoja na kiwango cha maji
yanayozalishwa kwa siku kutotosheleza mahitaji,
Upotevu wa maji na Uchakavu wa Miundombinu.
Katika kupambana na changamoto hizo
DAWASCO ikishirikiana na DAWASA na Wizara
ya Maji, imeanza hatua za utekelezaji wa mikakati
ya kuondoa kero inayowakabili watumiaji wa
huduma kwa kuanza kwa ujenzi wa miradi
ya kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita
za ujazo 300,000 mpaka kufi kia mita za ujazo
710,000 kwa siku, ikizingatiwa kuwa makadirio
ya matumizi ya maji kwa siku ni mita za ujazo
450,000 kwa siku.
Mkakati huu unahusisha upanuzi wa mitambo
ya kuzalisha Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini,
Uchimbaji wa visima 20 katika maeneo ya Kimbiji
na Mpera, ujenzi wa Bwawa la Kidunda Mkoani
Morogoro na mradi wa kupunguza upotevu wa
maji toka asilimia 48 hadi asilimia 20.
Kazi ya upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini
inaendelea na baada ya kukamilika utaongeza
uzalishaji toka mita za ujazo 182,000 hadi mita
za ujazo 270,000 kwa siku.Upanuzi wa Mtambo
wa Ruvu Juu utaongeza uzalishaji toka mita
za ujazo 81,000 mpaka za ujazo mita za ujazo
196,000 kwa siku, wakati visima virefu peke yake
vitaweza kuzalisha mita za ujazo 260,000 kwa
siku. Mipango yote hii ipo katika utekelezaji na
hivyo kuweka tumaini la kutoa huduma bora na
ya uhakika ifi kapo Disemba 2014.
Ujenzi wa bwawa la kuhifadhia Maji Kidunda
Mkoani Morogoro wenye uwezo wa kuhifadhi
hektomita za ujazounalenga kuhakikisha
upatikanaji wa Maji katika vipindi vyote vya majira
ya mwaka. Hii itasaidia kukabiliana na tatizo la
kupungua kwa kina cha Maji katika mto Ruvu
hasa kipindi cha Kiangazi.
Tunawasihi wananchi waendelee kuitunza,
kuilinda na kuhifadhi Miundombinu yote ya maji
iliyopo katika maeneo yao
Katika utoaji wa huduma za kila siku, Shirika
linakabiliana na changamoto kubwa zifuatazo;
Gharama za kubwa nishati ya umeme na
madawa ya kutibu maji, maji kutotosheleza
mahitaji, upotevu wa maji, hujuma kwenye
miundombinu ya maji safi na majitaka kama vile
wizi wa maji na wizi wa mifuniko ya chemba za
majitaka. Pia wateja kutolipia ankara kwa wakati,
maji kupatikana kwa mgawo na maeneo mapya
kutokuwa mabomba ya usambazaji.
Katika kukabiliana na changamoto hizi za
uendeshaji, DAWASCO inasimamia na
kutekeleza majukumu yake kwa kuzishirikisha
Serikali za mitaa, wateja na wadau wengine
wa Maji katika kulinda, kutunza na kuhifadhi
Miundombinu ya Maji ili isiharibiwe au kuibiwa.
Kwakuwa asilimia 13 tu ya jiji la Dar es Salaam
ndio inayopata huduma ya majitaka na hivyo
ipo mikakati ya kupanua huduma hii muhimu na
ustawi wa jiji la Dar es Salaam. Katika hili Shirika
lina mkakati wa kujenga mitambo maalumu ya
kusafi sha Majitaka katika maeneo ya Jangwani,
Kurasini na Mbezi Beach.
Mpango huu pia utahusisha ukarabati wa
miundombinu ya majitaka na kuendeleza juhudi
za kukemea na kuchukua hatua za kisheria
kwa wezi wa mifuniko ya chemba za majitaka
zinazosababisha kuziba na Majitaka kufurika
barabarani, kusababisha hatari kwa watumiaji wa
barabara na pia ni hatari kwa afya za wakazi.
DAWASCO inadhamiria kuleta mabadiliko ya
kiutendaji na kuboresha huduma kwa Umma
wa Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kibaha na
Bagamoyo Mkoani Pwani. DAWASCO ya sasa
imejipanga kutimiza wajibu wake kwa kusimamia
mikakati iliyojiwekea na hivyo wito unatolewa kwa
jamii kutimiza wajibu wake kwa kulipa ankara za
Maji kila mwezi ili kuliwezesha Shirika kuendesha
shughuli zake kwa ufanisi zaidi. DAWASCO
TUTAKUFIKIA
 
 

No comments:

Post a Comment