Friday, June 16, 2017

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017:MBEYA
















 Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw. Musa Mapunda (wa pili kutoka kushoto)
akieleza majukumu ya jiji hilo wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji
hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
 Kaimu
Katibu Tawala wa Jiji la Mbeya Bw.Nyasembwa Sivangu akisoma taarifa ya
Jiji la Mbeya  wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bi.Susan Mlawi (wa pili kutoka kulia) ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia ni 
Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba.
 Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bi.Susan Mlawi akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa
viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya alipofanya ziara ofisini hapo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma 2017.
 Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika
mapema leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma
2017.
 Mkurugenzi
Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky
Kiliba,akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za OPRAS zinazopima
utendaji kazi wa mtumishi.
 Mmoja
wa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya akiuliza swali wakati wa
ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Bi.
Susan Mlawi (hayupo pichani) jijini hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Viongozi
wa Halmashauri ya Jiji la mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais,Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (hayupo
pichani) alipofanya ziara jijini hapo mapema leo lengo ikiwa ni
kusikiliza changamoto wanazokutana nazo waajiri katika Utumishi wa Umma
na kuzipatia ufumbuzi. Ziara hiyo ni moja ya Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2017.

WAZIRI MKUU AMEWATAKA MAAFISA MIFUGO WABADILIKE














WAZIRI MKUU AMEWATAKA MAAFISA MIFUGO WABADILIKE

WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa mifugo wote wa wilaya na mikoa
wabadilike ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake kwenye pato la
Taifa.
“Katika ziara zangu za mikoani nimekuwa
nikionesha kutoridhishwa kwangu na utendaji kazi wenu, na hasa jinsi
tunavyoendesha ufugaji hapa nchini. Mmeacha kazi ya kuwaongoza wafugaji,
wanafanya wanavyotaka. Tunahitaji kuona mabadiliko makubwa katika sekta
hii,” amesema. 
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 15, 2017) wakati akizungumza na
maafisa mifugo kutoka wilaya zote na mikoa yote wanaohudhuria kikao
alichokiitisha ili wajadili namna wanavyoweza kubadili uchungaji na kufanya uwe ufugaji. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu amesema takwimu
za mwaka 2016 zinaonyesha Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika na ya
11 duniani kwa ufugaji, ikiwa na ng’ombe takriban milioni 24, nyuma ya
Ethiopia yenye ng’ombe milioni 54 na Sudan yenye ng’ombe 41.
“Wakati
sekta ya mifugo inatoa mchango usiozidi asilimia 10 kwenye Pato la
Taifa, wenzetu Ethiopia sekta hiyo hiyo inachangia asilimia 14 kwenye
pato lake na asilimia 16 ya fedha za kigeni. Nchi kama Botswana na
Namibia, nazo zinafanya vizuri kwenye sekta ya mifugo, pamoja na kwamba
wana mifugo michache, na eneo dogo la ardhi,” amesema.
“Ni
lazima tuanze kufikiri tofauti na kujitathmini kama kweli tunawatendea
haki Watanzania waliogharamia elimu yetu na wanaoendelea kutulipa
mishahara. Ningependa kupata ufahamu wenu wa kitaalam mna mipango gani
kuinua sekta hii kwa kuwafanya wafugaji wa Kitanzania wawe wafugaji
wanaotumia utaalam na hatimaye wao wenyewe na Taifa zima linufaike kwa
kupunguza umaskini,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu amewataka maafisa hao wabadili mitazamo yao na waache kufanya kazi
kwa mazoea. “Ni lazima mtafute ufumbuzi wa kudumu kuhusu utatuzi wa
migogoro baina ya wakulima na wafugaji; na wafugaji na wahifadhi wa
mapori tengefu au mapori ya akiba.”
Amewataka
wajipange kuongeza uzalishaji wa mitamba na kuweka mazingira wezeshi
kwa sekta binafsi kuendelea kuzalisha mitamba ili kuhamasisha ufugaji wa
kisasa. Na pia watenge, wapime na kuwamilikisha wafugaji maeneo ya
ufugaji.
Amesema
ili kukuza sekta hiyo hawana budi kutoa elimu ya matumizi ya teknoljia
ya uhamilishaji, kuendeleza na kukuza masoko ya mifugo na mazao yake kwa
kujenga viwanda. “Afisa mifugo ni lazima ujue kwenye Halmashauri yako
kuna minada mingapi na inafanyika wapi.  Kwenye bajeti hii, tumeondoa
kodi ya makanyagio, naamini hii itaongeza chachu ya wafugaji kupelekea
mifugo yao minadani,” amesema. 
Amewataka
pia waendelee kuimarisha huduma za ugani katika ngazi za kata na vijiji
na kuhakikiasha wanaanzisha mashamba darasa ya mifugo. “Jipangeni
kuanzisha mashamba darasa ya malisho katika kila Halmashauri. Kila eneo
mnaweza kuwa na shamba darasa kwa kuchagua mfugaji mmoja au wawili ili
wawe ndiyo mashamba darasa kwa wenzao,” amesema.
Mkutano
huo ambao umehudhuriwa na maafisa mifugo wa wilaya 185 na Maafisa
Tawala Wasaidizi wa Mikoa (wanaoshughulikia masuala la mifugo) zaidi ya
20, umehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles
Tizeba, na Naibu Waziri wake, Bw. Willian Tate Ole Nasha, Makatibu Wakuu
wa Wizara za Kilimo na TAMISEMI, Wakuu wa Mapori ya Akiba, Wakurugenzi
wa Wizara ya Viwanda na Biashara na taasisi zinashughulika na maliasili;
na wakuu wa vyuo vya wanyamapori.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Waziri wa Nchi (OR –
TAMISEMI), Bw. George Simbachawene alisema migogoro na chuki vinatokea
kwa sababu wahusika hawajaoa​ ​nisha mifugo kama rasilmali na kuzifungamanisha na uchumi wa watu wengine.


Tuchukue
mfano, mtu akiwa na ng’ombe 1,000 katika eneo fulani. Kama uzalishaji
wake ukioanishwa na uchumi wa eneo husika, mafanikio lazima yatakuwa ni
ya eneo lile na siyo ya mtu binafsi,” alisema.

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFAURU KATIKA MASOMO YA KEMIA NA BAIOLOJIA

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFAURU KATIKA MASOMO YA KEMIA NA BAIOLOJIA 





01
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa
Mohamed Bakari akizungumza katika hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia
Wanafunzi na Waalimu wao waliofanikiwa kufanya vizuri zaidi katika
masomo ya Kemia na Baiolojia kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha nne
mwaka 2015 na kidato cha sita mwaka 2016 iliyofanyika leo katika makao  
makuu ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali Ocean Road jijini Dar es
salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
1
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa
Mohamed Bakari akikabidhi zawadi kwa Mwanafunzi Congcong Wane wa shule
ya sekondari Fedha  katika hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia Wanafunzi
na Waalimu wao waliofanikiwa kufanya vizuri zaidi katika masomo ya
Kemia na Baiolojia kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2015
na kidato cha sita mwaka 2016 iliyofanyika leo katika makao makuu ya
Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)Ocean Road jijini Dar es salaam, Congcong
pia ndiye mwanafunzi aliyefauru vizuri kitaifa katika somo la Kiswahili
na ana uwezo mkubwa wa kuongea kiswahili, wanaoshuhudia tukio hilo wa
pili kutoka kushoto ni Samwel Manyere na wa pili kutoka kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa
David Ngassapa.
2
Mwanafunzi Congcong Wane wa shule
ya sekondar Fedha akihijiwa na mwandishi wa habari wa Kituo cha
Televisheni cha Swahili Steven Mumbi mara baada ya kupokea zawadi yake.
3 4

Wanafunzi wengine pia wakipokeza zawadi zao.

5
6
Wakurugenzi na mameneja wa Wakala wa Mkemia mkuu wa Serikali (GCLA)wakiwa katika hafla hiyo
7
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha
nne na sita kutoka shule mbalimbali nchini waliofanya vizuri kwenye
masomo ya Kemia na Baiolojia wakiwa katika hafla hiyo.

8
Profesa Samwel Manyere Mkemia
Mkuu wa Serikali akizungumza katika hafla hiyo wakati akimkaibisha
mwenyekiti wa bodi ili kuzungumza.

9
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.

10
Baadhi ya walimu na wazazi waliohudhurika katika hafla hiyo.

11
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa David Ngassapa akimkaribisha
mgeni rasmi Profesa Mohamed Bakari  ili kuzungumza katika hafla hiyo.

  13
Mmoja wa wanafunzi waliofanya
vizuri kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia akitoa shukurani kwa Mkemia
mkuu wa Serikali kwa kuwatambua na kuthamini juhudi zao kutokana na
kitondo cha kuwazawadia wanafunzi hao.
14
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa David Ngassap, Mganga Mkuu wa
Serikali Profesa Mohamed Bakari na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa 
Samwel Manyere wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliozawadiwa
kuangalia picha zaidi shuka chini.
15 16 17
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa 
Samwel Manyere akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa wakala huo mara
baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwakabidh zawadi wanafunzi hao. Picha na Ismail Mang'ola

WATANO WADAKWA KWA KUMILIKI KIWANDA CHA KUGHUSHI NYARAKA ZA UHAMIAJI, HATI ZA KUSAFIRIA, VISA NA MASHINE ZA RISITI ZA KIELEKTRONIKI (EFDS) DAR.














WATANO WADAKWA KWA KUMILIKI KIWANDA CHA KUGHUSHI NYARAKA ZA UHAMIAJI,
HATI ZA KUSAFIRIA, VISA NA MASHINE ZA RISITI ZA KIELEKTRONIKI (EFDS)
DAR.

 Wazee waliokamatwa ni
Hemed Ali Mchepe(56), Edga Samson Mwafongo(55), Huruma Mwakidete(57), David
Tumpange (64), At human Mohammed (61) na Simon Joseph Veso (62).
 Vifaa vinavyotumika kughushi nyaraka
ambavyo vimekamatwa.
Kamishana wa
usimamizi wa mipaka idara ya Uhamiaji Tanzania, Samwel Magweiga (pichani),
amepiga marufuku Mawakala wanaojihusisha na shughuli za uhamiaji na kuwataka
waache mara moja kufanya hivyo na kuwataka wananchi wanaohitaji huduma hiyo
kufika ofisi husika ya uhamiaji.
 
Na Mwandishi Wetu

Kamishana Magweiga
ametoa wito huo leo, wakati akizungumzia ukamatwaji wa watu watano wenye umri
wa kati ya miaka 55 na 64 ambao walikutwa wakimiliki ofisi na mitambo ya
kughushi nyaraka mbalimbali ikiwamo ya kughushi miradi ya maendeleo ya Serikali
na machine za risiti za kielektroniki (EFDs).
Kufuatia ukamataji
huo, Kamishna Magweiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa idara ya
Uhamiaji ili kudhibiti mianya ya watu wanaojihusisha na kughushi nyaraka za
aina mbalimbali kwa kuwa zinapelekea uhujumu wa uchumi.



Mapema wiki hii,
makachero kutoka ofisi za uhamiaji baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasalimia
wema kuhusu kuwepo kwa hujuma hiyo, walifanya msako na kuwakamata wazee watano
ambao ofisi yao ipo eneo la Bibi Titi Mohammed kiwanja namba 16/47 lililopo
Wilaya ya Ilala mtaa wa Mtendeni.

"Kuna magenge ya
wahalifu huko mitaani ambao wanafanya kazi kwa niaba ya serikali, hawa ni
wahujumu uchumi, ni lazima wafichuliwe",amesisitiza Kamishna Magweiga.

Ameongeza kuwa,
nyaraka hizo za mara nyingi zimekuwa zinatumika kuchukua hati za kusafiria,
mikopo benki na kupelekea benki husika kupata hasara na serikali kukosa mapato.

Amesema
 upelelezi dhidi ya watuhumiwa hao umekamilika na siku yoyote watapelekwa
mahakamani ila badoa wanahitaji kujua mtandao wao ni mkubwa kiasi gani na upo
hapa nchini pekee ama na nje ya nchi.

Wakielezea jinsi
walivyokamatwa mbele ya Kamishana mzee David Tumpange alikubali kuwa yeye ni
mmiliki wa ofisi iliyokutwa na nyaraka hizo za kughushi iliyopo eneo la
barabara ya Bibi Titi Mohammed na kwamba yeye hashughuliki nayo alimkabidhi
ndugu yake Huruma Mwakidete.

Aliongeza kuwa, kwa
sasa yeye anajishughulisha na masuala ya ujenzi na siku ya tukio, alikwenda
kwenye ofisi yake hiyo kwa ajili ya kumsalimia ndugu yake huyo aliyemkabidhi
ofisi na vyote vilivyokutwa humo havitambui.

Huruma Mwakidete
ambaye ni mstaafu wa Kampuni ya Bia ya TBL na ndiye alikabidhiwa ofisi hiyo na
David, yeye alikubali kuendesha ofisi hiyo na kwamba ofisi hiyo ni ofisi huru
na inashughulika na mambo mbalimbali ikiwamo ujenzi.

Aliongeza kuwa
nyaraka zinazodaiwa za kughushi zilizokutwa ndani ya boxi katika ofisi yao
hazitambui na wala hajui zilikopatikana.

Edga Samson alisema
ofisi hiyo siyo yake, hausiki nayo ila alipita siku hiyo alipita ofisini hapo
kwa ajili ya kumuona rafiki yake Huruma Mwakidete.

Hemed Mchepe yeye ni
mstaafu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yeye alikana kuhusika na ofisi
hiyo wala nyaraka zilizokamatwa na kwamba alifika ofisini hapo kwa ajili ya
kusalimia marafiki zake na kusoma gazeti.

Watuhumiwa hao
walikamatwa na nyaraka mbali mbali za kughushi zikiwamo fomu mbalimbali za
Idara ya Uhamiaji Tanzania zikiwemo za kuomba hati za kusafiria, VISA, vibali
vinavyowaruhusu raia wa nje kuishi nchini na kufanya kazi, fomu ya shahada ya
dharura ETD.

Vingine ni, vyeti vya
kughushi vya ndoa na taraka kutoka Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza
la waislamu Tanzania (Bakwata), Karatasi za EFDs za manispaa, stakabadhi za
kutoza ushuru katika halmashauri mbalimbali ikiwamo ya Temeke.

Vingine ni vyeti vya
vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, vyeti vya kumaliza elimu ya msingi,
kidato cha nne, vyeti vya elimu ya juu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
matokeo yake.

Pia walikutwa na
nyaraka za uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma zinaoonyesha ni halali na
zimetolewa na Baraza Mitihani Tanzania, nyaraka za kughushi za makubaliano ya
miradi mbalimbali ya maendeleo ya Serikali ikiwamo mradi wa Wilaya ya Mafia
wenyewe zabuni namba LGA 008/2016/2017/W/15 package II.

Mbali na nyaraka hizo
za kughushi pia walikutwa na leseni za utalii za kughushi zinazotolewa na bodi
ya Utalii nchini, Tin namba na nyaraka za ulipaji wa kodi zinazotolewa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vyeti vya kughushi vya kuzaliwa, matangazo ya
kuzaliwa ya mtoto yanayotolewa na Idara ya Msajili Mkuu wa Vizazi na vifo,
Stakabadhi za halmashauri za kukusanya ushuru, vitambulisho vya Mkazi, hati
mikiliki, nyaraka za utambulisho wa utumishi wa umma wa halmashauri ya Manispaa
ya Temeke, nyaraka za kupotelewa na kitu zinazotolewa na kes jeshi la polisi.

Pia walikutwa na
mihuri ya kughushi ya benki ya Exim tawi la mnara wa saa na tawi la Namanga,
muhuri wa mkuu wa Shule ya sekondari ya Jamuhuri Dodoma, makampuni mbalimbali
na mihuri ya Halmashauri mbalimbali na Kata ikiwamo ya Mtendeni.

KATIBU WA BUNGE DKT. KASHILILAH AONGOZA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA BUNGE LEO UKUMBI WA SPIKA MJINI DODOMA

KATIBU WA BUNGE DKT. KASHILILAH AONGOZA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA BUNGE LEO UKUMBI WA SPIKA MJINI DODOMA

 Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akiongoza
kikao cha Menejimenti ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika
Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Utumishi wa
Bunge wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akizungumza katika kikao hicho
kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

Wednesday, June 14, 2017

True value Media:    DC BYAKANWA ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOLEA

DC BYAKANWA ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOLEA





Mkuu
wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na
usalama wilaya ya Hai katika lango la kuingilia katika shamba la Kilimo
cha Kisasa la Mboga Mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd lililopo Nshara
Machame.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,akiwaongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya
wilaya Hai ,pamoja na askari Mgambo wakiingia katika shamba la Kilimo
cha Kisasa cha Mboga mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Shamba la Kilimo cha Kisasa,(Green House) lililopo Nshara Machame wilaya ya Hai la Kilimanjaro Vegees Ltd .
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama
wilaya ya Hai,wakiwa katika moja ya shamba hilo pamoja na asakari
polisi wenye silaha wakiondoa miundo mbinu ya umwagiliaji pamoja na
unyunyiziaji wa dawa .
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza katika eneo hilo wakati
zoezi la kuondoa miundo mbinu katika eneo hilo ikiendelea.Zoezi hilo
limefanyika kwa kile kinachodaiwa shughuli za kilimo kufanyika kando ya
mto kinyume cha sharia.
Sehemu ya Shamba la Strawberry kabla ya kuondolewa miundo mbinu.
Askari
Mgambo wakiondoa miundo mbinu ya umwailiaji katika shamba la Kilimoa
cha Kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wajimbo la
Hai,Freeman Mbowe.
Mipira maalumu iliyokuwa ikitumika katika umwagiliaji ikiwa imekatwa katwa .
Asakari Mgambo wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu.
Mkuu  wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akifuatilia zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji katika shamba hilo.
Mkuu
wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akisaidia katika uondoshaji wa
miondo mbinu katika shamba la kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd
linalomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Askari Mgambo wa kikata mipira kwa panga .
Zao la Strawberry ni moja wapo ya mazao yanyolimwa kisasa katika shmaba hilo.
Sehemu ya Mazao ambayo tayari yameanza kukomaa katika shamba hilo.
Kilimo cha kisasa cha zao la Nyanya pia kimekuwa kikifanyika katika shamba hilo.
Baadhi ya Green House zikiwa zimeondolewa wavu maalumu wa kuzuia wadudu kuingia ndani.

Na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.