Friday, June 16, 2017

WATANO WADAKWA KWA KUMILIKI KIWANDA CHA KUGHUSHI NYARAKA ZA UHAMIAJI, HATI ZA KUSAFIRIA, VISA NA MASHINE ZA RISITI ZA KIELEKTRONIKI (EFDS) DAR.














WATANO WADAKWA KWA KUMILIKI KIWANDA CHA KUGHUSHI NYARAKA ZA UHAMIAJI,
HATI ZA KUSAFIRIA, VISA NA MASHINE ZA RISITI ZA KIELEKTRONIKI (EFDS)
DAR.

 Wazee waliokamatwa ni
Hemed Ali Mchepe(56), Edga Samson Mwafongo(55), Huruma Mwakidete(57), David
Tumpange (64), At human Mohammed (61) na Simon Joseph Veso (62).
 Vifaa vinavyotumika kughushi nyaraka
ambavyo vimekamatwa.
Kamishana wa
usimamizi wa mipaka idara ya Uhamiaji Tanzania, Samwel Magweiga (pichani),
amepiga marufuku Mawakala wanaojihusisha na shughuli za uhamiaji na kuwataka
waache mara moja kufanya hivyo na kuwataka wananchi wanaohitaji huduma hiyo
kufika ofisi husika ya uhamiaji.
 
Na Mwandishi Wetu

Kamishana Magweiga
ametoa wito huo leo, wakati akizungumzia ukamatwaji wa watu watano wenye umri
wa kati ya miaka 55 na 64 ambao walikutwa wakimiliki ofisi na mitambo ya
kughushi nyaraka mbalimbali ikiwamo ya kughushi miradi ya maendeleo ya Serikali
na machine za risiti za kielektroniki (EFDs).
Kufuatia ukamataji
huo, Kamishna Magweiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa idara ya
Uhamiaji ili kudhibiti mianya ya watu wanaojihusisha na kughushi nyaraka za
aina mbalimbali kwa kuwa zinapelekea uhujumu wa uchumi.



Mapema wiki hii,
makachero kutoka ofisi za uhamiaji baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasalimia
wema kuhusu kuwepo kwa hujuma hiyo, walifanya msako na kuwakamata wazee watano
ambao ofisi yao ipo eneo la Bibi Titi Mohammed kiwanja namba 16/47 lililopo
Wilaya ya Ilala mtaa wa Mtendeni.

"Kuna magenge ya
wahalifu huko mitaani ambao wanafanya kazi kwa niaba ya serikali, hawa ni
wahujumu uchumi, ni lazima wafichuliwe",amesisitiza Kamishna Magweiga.

Ameongeza kuwa,
nyaraka hizo za mara nyingi zimekuwa zinatumika kuchukua hati za kusafiria,
mikopo benki na kupelekea benki husika kupata hasara na serikali kukosa mapato.

Amesema
 upelelezi dhidi ya watuhumiwa hao umekamilika na siku yoyote watapelekwa
mahakamani ila badoa wanahitaji kujua mtandao wao ni mkubwa kiasi gani na upo
hapa nchini pekee ama na nje ya nchi.

Wakielezea jinsi
walivyokamatwa mbele ya Kamishana mzee David Tumpange alikubali kuwa yeye ni
mmiliki wa ofisi iliyokutwa na nyaraka hizo za kughushi iliyopo eneo la
barabara ya Bibi Titi Mohammed na kwamba yeye hashughuliki nayo alimkabidhi
ndugu yake Huruma Mwakidete.

Aliongeza kuwa, kwa
sasa yeye anajishughulisha na masuala ya ujenzi na siku ya tukio, alikwenda
kwenye ofisi yake hiyo kwa ajili ya kumsalimia ndugu yake huyo aliyemkabidhi
ofisi na vyote vilivyokutwa humo havitambui.

Huruma Mwakidete
ambaye ni mstaafu wa Kampuni ya Bia ya TBL na ndiye alikabidhiwa ofisi hiyo na
David, yeye alikubali kuendesha ofisi hiyo na kwamba ofisi hiyo ni ofisi huru
na inashughulika na mambo mbalimbali ikiwamo ujenzi.

Aliongeza kuwa
nyaraka zinazodaiwa za kughushi zilizokutwa ndani ya boxi katika ofisi yao
hazitambui na wala hajui zilikopatikana.

Edga Samson alisema
ofisi hiyo siyo yake, hausiki nayo ila alipita siku hiyo alipita ofisini hapo
kwa ajili ya kumuona rafiki yake Huruma Mwakidete.

Hemed Mchepe yeye ni
mstaafu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yeye alikana kuhusika na ofisi
hiyo wala nyaraka zilizokamatwa na kwamba alifika ofisini hapo kwa ajili ya
kusalimia marafiki zake na kusoma gazeti.

Watuhumiwa hao
walikamatwa na nyaraka mbali mbali za kughushi zikiwamo fomu mbalimbali za
Idara ya Uhamiaji Tanzania zikiwemo za kuomba hati za kusafiria, VISA, vibali
vinavyowaruhusu raia wa nje kuishi nchini na kufanya kazi, fomu ya shahada ya
dharura ETD.

Vingine ni, vyeti vya
kughushi vya ndoa na taraka kutoka Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza
la waislamu Tanzania (Bakwata), Karatasi za EFDs za manispaa, stakabadhi za
kutoza ushuru katika halmashauri mbalimbali ikiwamo ya Temeke.

Vingine ni vyeti vya
vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, vyeti vya kumaliza elimu ya msingi,
kidato cha nne, vyeti vya elimu ya juu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
matokeo yake.

Pia walikutwa na
nyaraka za uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma zinaoonyesha ni halali na
zimetolewa na Baraza Mitihani Tanzania, nyaraka za kughushi za makubaliano ya
miradi mbalimbali ya maendeleo ya Serikali ikiwamo mradi wa Wilaya ya Mafia
wenyewe zabuni namba LGA 008/2016/2017/W/15 package II.

Mbali na nyaraka hizo
za kughushi pia walikutwa na leseni za utalii za kughushi zinazotolewa na bodi
ya Utalii nchini, Tin namba na nyaraka za ulipaji wa kodi zinazotolewa na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vyeti vya kughushi vya kuzaliwa, matangazo ya
kuzaliwa ya mtoto yanayotolewa na Idara ya Msajili Mkuu wa Vizazi na vifo,
Stakabadhi za halmashauri za kukusanya ushuru, vitambulisho vya Mkazi, hati
mikiliki, nyaraka za utambulisho wa utumishi wa umma wa halmashauri ya Manispaa
ya Temeke, nyaraka za kupotelewa na kitu zinazotolewa na kes jeshi la polisi.

Pia walikutwa na
mihuri ya kughushi ya benki ya Exim tawi la mnara wa saa na tawi la Namanga,
muhuri wa mkuu wa Shule ya sekondari ya Jamuhuri Dodoma, makampuni mbalimbali
na mihuri ya Halmashauri mbalimbali na Kata ikiwamo ya Mtendeni.

No comments:

Post a Comment