Maaskofu wakiwa wamenyanua picha
ya rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya maombezi.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza askofu Dkt. Charles Gadi (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza
kuhusu jukumu la rais John pombe Magufuli kupiga vita matumizi na uuzwaji wa
dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa kuunga
mkono juhudi za rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi hasa katika zozi gumu la kupiga vita
madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa Good News For All Ministry , askofu Dkt.
Charles Gadi kwa niaba ya madhehebu mbalimbali, amesema utendaji wa rais John
Pombe Magufuli unapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania kwani vita ya dawa za
kulevya ni kubwa na ngumu kuzizibiti lakini kwa mwenendo alioanzia mhe rais ni
mzuri na atashinda vita hivyo.
Aidha askofu Dkt. Charles Gadi aliongoza
jopo la maaskofu wenzake kumuombea rais Magufuli, taifa pamoja na viongozi
wengine.