Wednesday, February 22, 2017

VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI WALIPOKUWA WAKIMUOMBEA RAIS MAGUFULI NA TAIFA KWA UJUMLA

Maaskofu wakiwa wameshika picha ya rais John Pombe  Magufuli kwa ajili ya maombezi maalumu.


Maaskofu wakiwa wamenyanua picha ya rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya maombezi.


askofu Dkt. Charles Gadi wa nne kutoka kushoto akiwaongoza maaskofu wenzake kuliombea taifa
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza askofu Dkt. Charles Gadi (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza kuhusu jukumu la rais John pombe Magufuli kupiga vita matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.
Watanzania wametakiwa kuunga mkono juhudi za rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi hasa katika zozi gumu la kupiga vita madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa Good News For All Ministry , askofu Dkt. Charles Gadi kwa niaba ya madhehebu mbalimbali, amesema utendaji wa rais John Pombe Magufuli unapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania kwani vita ya dawa za kulevya ni kubwa na ngumu kuzizibiti lakini kwa mwenendo alioanzia mhe rais ni mzuri na atashinda vita hivyo.
Aidha askofu Dkt. Charles Gadi aliongoza jopo la maaskofu wenzake kumuombea rais Magufuli, taifa pamoja na viongozi wengine.


No comments:

Post a Comment