Thursday, March 2, 2017

True value Media: Maaskofu wakiwa wameshika pichaya rais John Pombe ...











 
Na Ismail Mang'ola, Dar
Kufuatia agizo kutoka ofisi ya Makamu wa Rais na Mazingira ikishirikiana na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka
ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  leo imefanya operesheni kwa baadhi ya
wasambazaji wa pombe za kali zinazofungashwa katika plasti maarufu kama
kiviroba ili kujiridhisha kama wameitikia wito wa kusitisha utengenezaji,
usambazaji na uuzaji wa pombe hizo.
Akiongea na vyombo vya habari
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi
amesema kuwa operesheni hiyo imeanza na wasambazaji, wauzaji na watumiaji huku
wakiendelea kupitia baadhi ya maombi ya wamiliki wa viwanda juu ya usitishaji
wa pombe hizo.
Aidha operesheni hiyo
imefanyika katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa kutembelea maghala
yanayohifadhi pombe hizo ili kujua idadi ya pombe ambazo bado zipo katika
maghala hayo pamoja na kufuatilia ikiwa wamiliki wa maghala hayo wametii amri
ya kusimamisha usambazaji wa Pombe hizo zilizofungiwa kuanzia Marchi 01, 2017.
Msimamizi wa ghala la Pombe
za Viroba  aina ya Kiroba Original lililopo Mabibo wilaya ya Kinondoni
 Mhina Rashid amesema kuwa akiba ya pombe hizo za viroba zilizobaki katika
maghala yao ni katoni 6600  za ujazo wa Ml 50 na katoni 4909 zenye ujazo
wa Ml100.
“Kwa sasa tumefunga maghala
na hakuna usambazaji wowote wa pombe aina ya kiroba unaofanyika hapa tunasubiri
taratibu za Serikali kujua nini cha kufanya kwa pombe ambazo bado zipo katika
maghala,” alifafanua Mhina Rashid.
Aliendelea kwa kusema kuwa
ikiwezekana Serikali iongeze muda wa matumizi ya pombe hizo kutokana na kuwa na
mzigo mkubwa katika maghala mengi yanayohifadhi pombe hizo.
Kwa upande wake, Afisa
Mwandamizi wa Viwango na Mkaguzi wa TBS Banza Suleiman amesema kuwa viroba
Original vina nembo ya TBS lakini kutokana na sheria mpya ambayo imepiga
marufuku matumizi ya pombe hizo hivyo wasambazaji hawaruhusiwi kusambaza pombe
hizo bali wanapaswa kusubiri maelekezo toka Serikalini.
Vile vile operesheni hiyo
imefanyika katika kiwanda cha Afro American kilichopo Mwenge ambao ni
watengenezaji wa pombe za viroba aina ya Zed, Royal na Dollors na kukuta zaidi
ya tani 5 ya pombe hizo.
Msimamizi wa kiwanda hicho
Muhandisi Sabra Voleti amesema kuwa wamesimamisha uzalishaji wa pombe za viroba
huku wakisubiri maelekezo toka Serikalini. Aidha amesema kuwa kiwanda hicho
kinaendelea na uzalishaji wa pombe ambazo vifungashio vyake ni vya chupa.
Kwa upande wake Mwanasheria
wa NEMC Manchare Heche Suguta amesema kuwa adhabu ya matumizi ya vifungashio
vya plastiki (Viroba) vinatofautiana kati ya mtengezaji, msambazaji, muuzaji na
mtumiaji. Aidha adhabu yake ni faini kati ya shilingi elfu 50 na Milioni 5 au
kifungo kisichopungua miaka 3.
Hivyo amewataka watanzania
kujiepusha na matumizi ya pombe hizo pamoja ikiwa ni pamoja na utengenezaji na
usambazaji wake.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
Manyara Februari, 2017 aliagiza pombe hizo kutoendelea kutumika kuanzia Marchi
1, 2017.


No comments:

Post a Comment